Alikiba na Jokate Siri Yafichuka

Mahusiano kati ya msanii Alikiba na aliyeaminika kuwa mpenzi wake Jokate Mwegelo, ambaye ni mwanamitindo na mjasiriamali anayetazamwa na dunia nzima, bado yanaendelea kwa upande wa kazi za sanaa, ambapo wawili hao ni mtu na bosi wake.

Jokate na Ali Kiba

Siri hiyo imetolewa na msanii Abby Skills ambaye pia ni mtu wa karibu na Alikiba na moja ya msanii ambaye yupo chini ya lebo ya muziki ya Alikiba, alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, na kusema kwamba Jokate yupo chini lebo ya Alikiba, ambayo pia yeye yupo.

“Mimi pia nipo chini ya lebo yake, Alikiba  ni bosi wangu, kuna Abdu Kiba, kuna Salim, kuna Heri, kuna Jojo Jokate”, amesikika Abby Skills akitoa siri hiyo ambayo hakutakiwa kuiweka wazi kwa mujibu wake mwenyewe.

Alikiba na Jokate waliwahi kuwa na tetesi kuwa na mahusiano ya kimapenzi, na hivi karibuni Alikiba alisikika akisema hadharani kwamba hana mahusiano na mwanamitindo huyo.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364