-->

Asilimia 61 Tanzania Kuwa Jangwa-Makamba

Takwimu zinaonyesha kwamba nchi ya Tanzania ipo hatarini kugeuka jangwa ambapo asilimia 61 ya maeneo ya nchi tayari yapo katika hatari zaidi ya ukame kutokana na ukataji miti hovyo.

January Makamba

Akizungumza ofisini kwake mjini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba amesema kwamba mikoa mbalimbali nchini imekwishaanza kuathirika na hali ya jangwa na ukame ambapo vyanzo vya maji tayari vimeshaanza kukauka, mifugo kufa ikiwa ni pamoja na upungufu wa mvua kutokana na ukataji wa miti kiholela na migogoro baina ya wafugaji na wakulima kutokana na kupungua kwa maeneo ya kilimo na malisho ya mifugo.

Waziri amesema kuwa ili kukabiliana na tatizo la ukame na jangwa nchini tayari serikali imekwishaweka mkakati wa kupanda miti milioni 280 kila mwaka kwenye maeneo ambayo yameathirika zaidi na jana hili la ukame.

Hata hivyo mikoa ambayo imekwisha athirika zaidi, Waziri ameitaja ni pamoja na na Singida, Dodoma, Shinyanga, Manyara, Simiyu, Geita na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Arusha.

Ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame Duniani ambayo inaadhimishwa ulimwenguni kote kila ifikapo tarehe 17 Juni, kauli mbiu ya mwaka huu ni “Ardhi ni Makazi yetu Tuitunze kwa Manufaa ya baadaye” (‘Our Land, Our Home, Our Future’).

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364