-->

Audio: P-Funk Atoa Sababu za Fid Q Kuwa Ndiye MC Mkali Duniani

Kwa P-Funk Majani, Fid Q ndiye MC mkali kuliko wote duniani. Si Tanzania, si Afrika pekee, Ngosha ni MC mkali dunia nzima.

Majani ameimbia Bongo5 kuwa cha kwanza ambacho watu wanapaswa waelewe ni kuwa kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake, ambapo kwa mtazamo wake Fid hana mpinzani duniani kwenye sekta ya uchanaji.

“I truly feel Fid Q as a lyrical monster,” Majani ameiambia Bongo5.

“Jana nimeichunguza mistari yake na kugundua kuwa that kid knows how to play with a pen and paper, now days anachezea iPhone kwenye lyrics. Punchline zake, very unique, ambazo hautakuja kumsikia msanii mwingine akatumia mistari kama ile. Watu wengi miaka nenda rudi wameshatambua hilo ila it took me time because I never used to pay attention to the lyrics that much and you know Swahili is not my first language ndio maana kuna utata saa zingine, but jana because for some reason I had to pay closer attention, nijaribu kuelewa kila kitu anachosema angeweza akawa ananichana hata mimi nisingejua. But the way he put the song together, made me realize his true capability and art, he is basically a one of a kind,” Majani amesisitiza.

“Fid is just another level, tumwache alivyo and he will always be the king.”

Majani amedai kuwa kitu kingine kinachomfanya Fid awe tofauti, ni ule uwezo wa kufanya kitu chake mwenyewe bila kuwa nakala ya mtu mwingine. “Kingine flow yale ni chafu, any beat I throw on him can attack and kill it,” amesisitiza.

“Third one is the love for the craft, he loves hip hop and hip hop loves him, he is the biggest thing there is when it comes to hip hop in Tanzania and even in East Africa naweza kusema, though kuna wengine wanaweza wakahate, but it is the truth, truth be told. But not to say that I don’t like Nas, Redman, Lupe, Andre 3000, Cuban Link, Busta Rhymes, Juelz Santana,J-Cole, wote nawakubali pia, but Fid ndio baba yao.”

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364