-->

Baba Mzazi wa Lulu Akataa Posa ya Lulu

Baba Mzazi wa muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael, Mzee Michael Kimemeta, amekataa kupokea posa ya binti yake huyo ambaye amekuwa akiwatoa udenda wanaume wengi kwa urembo wake.

“Niko Na Baba Mkweeee?ooopssss I mean Baba Angu??hadi vidole sikuhizi havina mfupa-L

Mzee Kimemeta amefunguka hayo alipokuwa akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba hatopokea posa ya mwanaume atakayekwenda kumuoa Lulu, kikubwa atakachoangalia ni furaha ya binti yake kwenye maisha yake.

“Suala la kuoana ni la watu wawili anayeoa na anaye olewa, yeyote atakayemleta sisi tunambariki, posa haiko kwenye msamiati wangu, siuzi mtoto, wala sitaki posa yoyote, posa yangu ni amani ndani ya nyumba yao, ndio posa watakayoniletea”, amsema Mzee Kimemeta.

Mzee Kimemeta ameonekana kuwa bega kwa bega na mwanaye kwenye kesi ya mauaji inayomkabili binti yake, iliyoanza kusikilizwa tena wiki hii.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364