-->

Bodi ya Filamu na Wadau wa Filamu Kuandaa Sera ya Sekta ya Filamu

Katibu wa Bodi ya filamu Bi. Joyce Fissoo amezidi kuonyesha dhamira kuu kwa wadau wa filamu baada ya kupigania uharakishaji wa uandaaji wa Sera ya Filamu ili kuwajengea wadau hao thamani ya kazi yao huku ikiwapa kipaumbele kikubwa katika kuwashirikisha wawakilishi wa wadau wa Filamu na kutoa maoni yao kupelekea kujenga tasnia yenye nguvu.

Katibu wa Bodi ya filamu Bi. J. Fissoo kushoto kwake Rais wa Taff Mwakifwamba

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano ya Bodi ya Filamu, imedai majadiliano hayo ni kwa ajili ya maandalizi ya sera mahususi itakayotoa mwongozo na kuendeleza sekta hiyo nchini.

Sekta ya filamu nchini imekuwa ikisimamiwa na Sera ya Utamaduni na Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza Na. 4 ya mwaka 1976 pamoja na kanuni zake. Kukosekana kwa sera mahususi ya filamu nchini kuliibua changamoto mbalimbali.

 

Changamoto hizo ni pamoja na kuwepo kwa filamu na michezo mingi ya kuigiza inayotayarishwa chini ya viwango, kutokuwepo kwa mitaji na uwekezaji wa kutosha, sekta ya filamu kutoendeshwa kibiashara, kukosekana kwa mifumo bora ya usambazaji, kutokuwepo kwa weledi na ubunifu wa kutosha, uharamia wa kazi za filamu.

Changamoto zilizoainishwa hapo juu zilibainika baada ya Bodi ya Filamu Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kufanya tafiti kuhusu hali halisi ya tasnia (situational analysis) na kuuwasilisha mbele ya kikao kazi cha wadau kilichofanyika tarehe 3 Oktoba, 2016 ukumbi wa uwanja wa Taifa.

Kwenye kikao hicho, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye, aliagiza uongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania na wizara yake kushirikiana pamoja kuhakikisha sera mahususi ya filamu inapataikana mapema iwezekanavyo.
Sera hiyo mahsusi ya filamu nchini inategemewa kuwa mwarobaini wa changamoto zinzoikabili sekta hiyo kwa muda mrefu sasa.

Ikumbukwe wadau wa tasnia ya filamu nchini wamekuwa wakilalamika kukosa mapato stahili yanayotokana na kazi zao, kushindwa kupata mitaji ya kuwawezesha kuwekeza miundo mbinu ya kisasa kwenye uzalishaji na mfumo hafifu wa kupambana na uharamia wa kazi zao.

 

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364