Category Archives: BongoFleva

VIDEO: Fid Q Afungukia Ishu ya Irene Uwoya ...

Post Image

Baada ya malkia wa filamu nchini Irene Uwoya kutoa kauli yake ya kuwa anapenda wanaume wagumu na kumtolea mfano Fid Q, rapper huyo amefunguka na kuzungumzia kauli ya muigizaji huyo. Akiongea na Bongo5 wiki hii, Fid Q amedai yeye siyo mwanaume mzuri lakini ana good look. “Mimi wakiitwa wanaume wabaya siwezi kwenda lakini pia wakiitwa […]

Read More..

Kilichomfanya Nahreel Apagawe kwa Aika, Hik...

Post Image

Msanii na producer Nahreel amefunguka sababu kubwa iliyomfanya kumpenda mpenzi wake Aika, ambaye wanaunda naye kundi la Navy Kenzo kuwa ni kutokana na uzuri wa mashavu yake na siyo hips wala kifua kizuri. Nahreel aliyasema hayo alipokuwa akiongea na EATV na kusema watu wengi wanadhani huenda alimpenda Aika kutokana na uzuri wake wa sura, uzuri wa […]

Read More..

Sakata la Q-Chief, Qs Mhonda Nyuma Yake Kun...

Post Image

HAINA tofauti sana na zile tetesi za usajili tunazo zisikia kwenye ulimwengu wa soka, ila safari hii tunazisikia kwenye tasnia ya muziki kufuatia mkongwe wa Bongo Fleva, Abubakary Katwila ‘Q Chief’ kuhusishwa kutua pale Wasafi Classic Baby (WCB). Uvumi huo umepata nguvu siku chache baada ya Q Chief kutangaza kuvunja mkataba na uongozi wake chini […]

Read More..

Baada ya Kumuita Nyani, Iyobo Amvaa Tena Ha...

Post Image

KIONGOZI wa madansa ambaye ni dansa tegemezi wa Wasafi Classic Baby (WCB) Mose Iyobo amefunguka kuwa yeye hana imani na Harmorapa na anashangaa anavyotajwa kila mahali kwani yeye hajawahi kusikia kazi yake yoyote hivyo hajui uwezo wake kimuziki. Iyobo aliendelea kwa kutoa povu kuwa yeye anamchukulia Harmorapa kama mtu aliyekurupuka kwenye muziki na hajui ni […]

Read More..

Ray C: Namtamani Ray Vanny

Post Image

Msanii wa muziki wa bongo fleva Ray C amefunguka na kusema anamtamani sana msanii kutoka katika label ya WCB Wasafi Ray Vanny na amekuwa akipenda sana kazi zake na kuzisikiliza, hivyo anatamani kufanya naye kazi hata moja tu. Ray C alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema anasikia Ray […]

Read More..

Alikiba Ampagawisha Waziri Nape Nnauye

Post Image

Msanii Alikiba ambaye leo ameachia remix ya wimbo wake wa ‘Aje’ ameonesha kumkosha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kiasi cha Waziri huyo kusema kuwa Alikiba ni kati ya wasanii wanaofanya ajisikie fahari kuwa Waziri Mhe. Nape Nnauye amesema hayo leo baada ya msanii huyo kukabidhiwa tuzo yake katika kituo kimoja […]

Read More..

Queen Darleen: Naumia Kuishi Bila Mpenzi

Post Image

MWANAMUZIKI anayefanya vizuri akiwa chini ya Lebo ya ‘WCB’, ‘Queen Darleen’ amefunguka kuwa anaumizwa sana na hali ya kuishi bila mpenzi jambo ambalo limekuwa likimuumiza sana katika maisha yake ya sasa maana yeye pia anahitaji kupenda na kupendwa kama walivyo watu wengine. Akichonga na Showbiz Xtra, Queen Darleen alisema kuwa, tangu aachane na mzazi mwenziye […]

Read More..

Masogange Apelekwa Kupimwa Utumiaji Madawa ...

Post Image

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro amesema mtuhumiwa Agness Gerald, maarufu Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuchukua vipimo vya damu ili kubaini kama anatumia dawa za kulevya. Masogange ambaye ni mrembo maarufu anayetamba katika video za wasanii mbalimbali wa bongo fleva alikamatwa na polisi juzi. […]

Read More..

Diamond Afungukia Ishu Yake ya Kuripoti Po...

Post Image

Msanii Diamond ameelezea kile kilitokea baada ya picha  kusambaa  zinazomwonyesha akihojiwa na jeshi la polisi. Muimbaji huyo amedai alienda polisi kujieleza kwa jeshi la usalama barabarani baada ya jeshi hilo kudaka clip yake ya video inayomwonyesha aliendesha gari huku akiwa hajavaa mkanda. Diamond ametoa taarifa hii kupitia ukurasa wake wa instagram Leo nilireport kituo kikuu […]

Read More..

Menina La Diva Ajifungua Mtoto wa Kiume

Post Image

MSANII wa Bongo Fleva aliyewahi kushiriki shindano la kusaka vipaji maarufu la Bongo Star Search (BSS), Menina, amejifungua mtoto wa kiume Februari 9 wiki iliyopita na jina la mtoto huyo bado halijafahamika. Aidha Menina aliyewahi kutamba na wimbo wake wa ‘Dream Tonight’ alitoa taarifa hiyo kupitia mtandao wake wa Instagram ambapo mastaa wenzake wakaendela kwa […]

Read More..

Watu Wanataka Kiki Kwa Jina Langu- Shilole

Post Image

ZUWENA Mohamed ‘Shilole’ analalamika akidai kuwa kwa sababu yeye ni msanii nyota wa filamu na muziki kuna watu wanataki kiki kupitia jina lake hata hivyo amelitambua hilo na atakuwa makini sana kila anaposikia jambo atafikiria alijibu au lah kwani akifanya hivyo anawatangaza wanaojinufaisha na jina lake. “Mimi ni super star kuna watu wanatumia jina langu […]

Read More..

Pombe Ilivyoharibu Muziki wa Nuruel

Post Image

Msanii wa bongo fleva Nuruel amesema ajali ya mguu aliyoipata miaka kumi iliyopita akiwa amelewa imekuwa ikimpa maumivu makali sana hali ya kumfanya kushindwa kufanya muziki vizuri kwa sasa. Akiongea kupitia eNewz ya EATV, amesema “Mguu wangu wa kushoto ulivunjika hali iliyonipelekea kupata mawazo sana na nikaachana na maswala ya muziki hali iliyonifanya nipotee kimuziki hata hivyo […]

Read More..

Mume wa Shamsa Ford, Chid Mapenzi Atakiwa ...

Post Image

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameamuru kukamatwa kwa mume wa muigizaji wa Bongo Movie Shamsa Ford, Chidi Mapenzi na kupelekwa polisi. ‘Kuna mtu anaitwa  Chid Mapenzi, huyo nataka  akachukuliwe sasa hivi nimkute  central’-Makonda aliagiza leo hii ikiwa ni muendelezo ya vita dhidi ya madawa ya kulevya. Chid Mapenzi ni mfanya biashara […]

Read More..

TID: Mimi ni Muathirika wa Dawa za Kulevya

Post Image

Mkali wa bongo Fleva, Khalid Mohamed maarufu kama TID, amekiri kuwa mmoja wa mastaa walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevya. Akizungumza leo kwenye mkutano ulioandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, TID amesema yuko tayari kubadilika. “Nimekuwa muathirika wa madawa ya kulevya, nimekuja kama kijana […]

Read More..

Ray C Afungukia Swala la Mahusiano Yake Kwa...

Post Image

Msanii Rehema Chalamila a.k.a Ray C ambaye ametamba kwenye anga la Bongo Fleva kwa siku nyingi, ameweka wazi kuwa kwa sasa hayuko kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote. Ray C ambaye amerejea kwenye game kwa kasi baada ya kutoka kwenye dimbwi ya matumizi ya dawa la kulevya, amefunguka hilo alipokuwa kwenye kipindi cha FNL […]

Read More..

Picha ya Mtoto wa Diamond,Nillan

Post Image

KWA mara ya kwanza, Mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnums ameianika sura ya mwanaye wa kiume, mdogo wake Tiffah aitwaye Nillan. Diamond na mpenzi wake Zari, wameiweka hadharani picha ya mtoto wao huyo ambaye leo Februari 11, 2017 anatimiza siku 40 tangu alipozaliwa nchini Afrika Kusini.

Read More..

Nilishakufa, Namshukuru Mungu-Ray C

Post Image

Msanii wa bongo fleva Ray C ambaye awali alikuwa mtumiaji wa madawa za kulevya amefunguka na kusema yeye alishakufa ila anamshukuru Mungu kwa wema wake na kumtoa katika janga hilo la dawa za kulevya. Ray C alisema hayo jana alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) na kusema leo hii yeye anasimama mstari wa […]

Read More..

TID Amtembelea Makonda Nyumbani, Afunguka H...

Post Image

Msanii wa kizazi kipya nchini TID ambaye siku kadhaa zilizopita alikuwa matatizoni akihusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya, amefunguka na kusema muziki bila madawa ya kulevya inawezekana. TID ambaye leo amekutana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda anasema kuwa amepata nafasi ya kukaa na kujadili na kiongozi huyo kuona […]

Read More..