Category Archives: BongoFleva

Nikki Mbishi Arusha Dongo kwa Nikki wa Pili

Post Image

Msanii wa Hip Hop Nikki Mbishi amemchana Nikki wa Pili na kumuambia kwamba aache kujiita msemaji wa wasanii kwa kuwa yeye ni msemaji wa kikundi kidogo cha wasanii wachache. Akiongea kupitia eNewz Nikki amesema Nikki wa Pili hapaswi kujiita msemaji wa wasanii kwa kuwa sanaa ya muziki ipo huru na kila mmoja anaposema ni msemaji wa wasanii siyo […]

Read More..

Prof. Jay Afungukia Muziki wa Hip Hop Bongo...

Post Image

Rapa mkongwe nchini Prof. Jay ambaye mwaka jana alitoa ngoma ya ‘hip hop singeli’ iliyokwenda kwa jina la ‘Kazi Kazi’ ameibuka na kusema wivu wa baadhi ya wasanii wa hip hop Bongo hauwezi kusaidia muziki wa hip hop kufika mbali. Licha ya wimbo huo wa ‘Kazi Kazi’ kufanya vizuri, na kuwepo kwa baadhi ya wasanii […]

Read More..

Wema Aalikwa Kwenye 40 ya Prince Nillan Jum...

Post Image

Kupitia kipindi cha LEO TENA kinachorushwa na CloudsFM Diamond Platnumz akiwa na mpenzi wake Zari, wamefunguka kumpa mwaliko staa wa bongo movie na mpenzi wa zamani wa Diamond,Wema Sepetu kwenye arobaini ya Mtoto wao Prince Nillan. “Namuomba Mungu Wema sepetu amalize tatizo lake salama na yeye tumemualika kwenye shughuli ya Prince NIllan Jumamosi, itakuwa ni […]

Read More..

Zari Afungukia Mipango ya Harusi Yake na Di...

Post Image

Zari The Bosslady amedai kuwa anataka harusi yake na Diamond Platnumz iwe kubwa na yenye gharama kuwahi kufanyika Afrika Mashariki. Hata hivyo, itafanyika baada ya kuwa wamefanya mambo ya muhimu zaidi ikiwemo kujijenga zaidi walivyo sasa. Akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Alhamis hii, Zari amedai kuwa suala la kufunga ndoa sio […]

Read More..

Alikiba na Diamond Mjipange – Abdukiba

Post Image

Msanii Abdukiba ambaye ni mdogo wa Alikiba amefunguka na kutoa ushauri kwa wasanii Alikiba na Diamond Platnumz kuwa wanapaswa kujipanga kimuziki na katika kazi zao kwani kuna vijana wengi wanajipanga kuchukua nafasi zao. Abdukiba alisema hayo kupitia kipindi cha ‘Ngaz kwa ngaz’ kinachorushwa na ting’a namba moja kwa vijana EATV, Abdukiba anasema wapo wasanii wengi […]

Read More..

Huyu Ndiye Mchumba wa Ommy Dimpoz?

Post Image

Msanii Ommy Dimpoz ambaye anafanya vyema na wimbo wake ‘Kajiandae’ wiki kadhaa zilizopita alifunguka na kusema ikifika wakati ataweka wazi suala la mahusiano yake kwa jamii, na kumuweka wazi mchumba wake ili watu wajue. Ommy Dimpoz alisema hayo kwenye kipindi cha eNewz cha EATV wiki kadhaa zilizopita, Ommy alifunguka na kuthibitisha kuwa kwa sasa yupo kwenye mahusiano na raia […]

Read More..

Picha: Harmorapa Amtembelea P-Funk Majani

Post Image

Msanii mchanga Harmorapa Jumatatu hii alimtembelea producer mkongwe wa Bongo Record, P-Funk Majani nakuzungumza naye mambo kadhaa kuhusu muziki. Hivi karibuni mtayarishaji huyo mkongwe alionyesha kupendezwa na harakati za rapper huyo ambaye amekuwa akizungumziwa kila kukicha. Rapper huyo baada ya kutembelea studio hapo na kukutana na mkongwe huyo alionyesha kufurahishwa huku akiwataka watu kuacha kuongea. […]

Read More..

VIDEO:Wasanii Wanaotuhumiwa Kujihusisha na ...

Post Image

Takriban watuhumiwa 10 wa dawa za kulevya ambao ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu asubuhi hii. Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani sasa ni wasanii Rommy Jones, TID, Babuu wa Kitaa, Nyandu Tozzy, Tunda (model wa kike), Lulu Diva, Recho, Joan, na […]

Read More..

Hatma ya Chege na Temba Sasa Hadharani

Post Image

Msanii kutoka TMK Wanaume Family, Chege Chigunda amesema yuko mbioni kukata kiu ya mashabiki wa ‘Chege na Temba’ kwani bada ya kutoa ngoma yake ya Kelele za Chura, ngoma inayofuata ni yake na swahiba wake Mh. Temba kutoka familia hiyohiyo ya Wanaume. Chege amelazimika kuweka wazi hatma ya Chge na Temba kutokana na kukumbana na […]

Read More..

Rachel, Tunda Waungana na Akina Wema, TID P...

Post Image

Video Queen maarufu hapa Bongo, Tunda pamoja na msanii wa Bongo Fleva, Winfrida Josephat  ‘Rachel’ wameripoti leo katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu tuhuma zinazowakabili za kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya. Tunda na Rachel wanaungana na wasanii wengine waliohojiwa na kushikiliwa kituoni hapo Ijumaa iliyopita ambao ni […]

Read More..

Bongo Fleva Someni Namba za Diamond

Post Image

UONGOZI wa kambi ya Wasafi umesema Diamond yuko bize sana na shoo kwa sasa. Kila kukicha Diamond Platinum ni lazima aangalie ratiba ya wapi atakuwepo. Inachosha japo inafurahisha na kutajirisha. Inachosha kwa sababu kama binadamu inabidi apumzike, ila inafurahisha kwa sababu mbali ya kufanya kitu anachokipenda, ila pia anazidi kuongeza uzito wa akaunti yake. Ni […]

Read More..

Mpoto Afunguka Sakata la Madawa ya Kulevya

Post Image

Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amefunguka kwa kusema kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao wanaunga mkono harakati za Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda za kupambana na biashara ya Madawa ya kulevya. Akiongea Jumapili hii katika kipindi cha runinga cha Jambo Tanzania cha TBC1, Mrisho Mpoto amedai […]

Read More..

Video: Haya Ndiyo Maisha Halisi ya Harmorap...

Post Image

MPAKA HOME: Msanii chipukizi anayekuja kwa kasi kwenye gemu la muziki wa kizazi kipya Bongo, Harmorapa aliyejipatia umaarufu kutokana na kufanana na msanii kutoka WCB, Harmonize, ameyaanika maisha yake ya kila siku na mpenzi wake ‘Wolper’ baada ya kutembelewa na MPAKA HOME ya Global TV Online. Ungana na mwandishi wetu, Imelda Mtema aliyemtembelea mpaka home kwake. […]

Read More..

Nape Afungukia Sakata la Wasanii wa ‘Unga’

Post Image

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameingilia kati na kutaka busara itumike katika zoezi la kutaja wasanii wanaohusika na dawa za kulevya linalofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Nape ametoa ushauri huo leo Mjini Dodoma wakati akizungumza na wanahabari kuhusu sheria mpya wa huduma za habari, ikiwa […]

Read More..

Hii Ndiyo Safari ya Muziki ya Ray Vanny

Post Image

Msanii Raymond alimaarufu kama Ray Vanny amefunguka na kuweka wazi safari yake ya muziki toka ameanza mpaka kufikia hatua kuingia chini ya usimamizi wa label ya WCB Wasafi chini ya Diamond Platnumz. Ray Vanny kupitia kipindi cha ‘Ngaz kwa ngaz’ kinachorushwa na ting’a namba moja kwa vijana anasema mwanzo kabisaa alianza kuandika, akaja kurap kisha […]

Read More..

Wema Sepetu, TID na Wenzao Waendelea Kushik...

Post Image

Wakati macho na masikio ya Watanzania wakisubiri kusikia hatma ya wasanii wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya, wasanii wanne waliofika Kituo Kikuu cha Polisi bado wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa bado wasanii hao Wema Sepetu, Dogo Hamidu, Khalid Mohamed (TID), […]

Read More..

New Video: Chege Ft Nandy – Kelele Za Chu...

Post Image

Msanii wa muziki Chege Chigunda ameachia video ya wimbo wake mpya, Kelele Za Chura akiwa amemshirikisha Nandy. Video imeandaliwa na Wanene Films chini ya director Destro.    

Read More..

Ray C: Viongozi Wamenipa Moyo Narudi Upya

Post Image

BAADA ya kutumbuiza kwa mafanikio katika kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa wa Dodoma (RCC) juzi, mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’, ameweka wazi kwamba yupo mbioni kurudi upya katika muziki wa ushindani kwa kuwa anaamini bado muziki wake una mashabiki wa kutosha. Ray C aliliambia MTANZANIA hayo baada ya kumaliza kutumbuiza nyimbo zake katika […]

Read More..