Category Archives: Other News

Gwajima Kumuombea Lissu

Post Image

Mchungaji Mchungaji Josephat Gwajima  wa kanisa la Ufufuo na Uzima amefunguka na kusema kuwa siku ya Jumapili atafanya maombezi maalum kwa afya ya Mbunge Tundu Lissu ambaye jana alipigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Dodoma nyumbani kwake. Mchungaji Gwajima amesema kuwa atatumia misa hiyo kulaani vikali kitendo cha kinyama alichofanyiwa Tundu Lissu na watu hao […]

Read More..

Rais Magufuli atoa tamko tukio la Lissu

Post Image

Rais John Magufuli amesikitishwa na taarifa alizozipata tukio la kupigwa kwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwa nyumbani kwake Dodoma leo na kuviagiza vyombo vya dola viwasake waliyofanya uhalifu huo. Rais Magufuli amesema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter jioni ya leo na kutaka vyombo vya usalama kuwatafuta watu waliofanya tukio hilo […]

Read More..

Magufuli ataka waliotajwa sakata la tanzani...

Post Image

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amewataka wateule wake wote waliotajwa katika ripoti za kamati zilizotathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya tanzanite na almasi kukaa pembeni kupisha vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi zake. Rais Magufuli amesema hayo leo Septemba 7, Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea […]

Read More..

Hashim Rungwe Ashikiliwa Polisi

Post Image

Dar es Salaam. Aliyekuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Hashim Rungwe anashikiliwa na polisi kwa siku nne sasa. Rungwe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Chaumma anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Mwanasiasa huyo anashikiliwa akituhumiwa kughushi nyaraka. Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Lazaro […]

Read More..

Polisi wafukua kaburi la dereva wa bodaboda

Post Image

Moshi. Mwili wa dereva wa bodaboda, Juma Hamis (26) umefukuliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi kubaini chanzo cha kifo chake. Hamis aliyekuwa mkazi wa Boma Mbuzi alizikwa katika makaburi ya Pasua mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Kufukuliwa kwa mwili huo kunatokana na amri iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi. Hamis alifariki dunia Julai 28 […]

Read More..

Charugamba Ammwagia Sifa Rose Mhando

Post Image

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili, Ussy Charugamba, amesema katika wakongwe kwenye tasnia hiyo, anamkubali zaidi Rose Mhando kwa kuwa amewaonyesha njia waimbaji wengi. Bosi huyo wa Ussy Production, ameliambia MTANZANIA kuwa anajiona mwenye bahati kufanya kazi na Rose Mhando kwa kumshirikisha kwenye wimbo wake unaoitwa ‘Wema’ ambao utakuwa kwenye albamu yake ya sita. “Rose Mhando […]

Read More..

Mahakama yafuta ushindi wa Uhuru Kenyata

Post Image

Mahakama ya juu nchini Kenya imefuta ushindi wa Rais Uhuru Kenyata kwa uchaguzi uliofanyika Agosti 8, 2017, na kutaka uchaguzi huo urudiwe.   Hukumu hiyo imetolewa leo na jopo la majaji 6 ilirushwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari nchini Kenya, imesema uchaguzi huo utarudiwa baada ya siku 60. Akisoma uamuzi huo Jaji Mkuu […]

Read More..

VIDEO:TANROADS Yadai Kutopata Zuio la Mahak...

Post Image

Dar es Salaam. Wakati Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kikilaani Kitendo cha Wakala wa Barabara Mkoa wa Dar es Salaam (Tanroads) kubomoa nyumba ambazo zina kinga ya mahakama, taasisi hiyo ya Serikali imeendelea na kazi hiyo kwa kuwa haijapewa zuio. Lakini meneja wa Tanroads wa Dar es Salaam, Julius Ndyamkama amesema hatua hiyo […]

Read More..

Hali ya Bulaya bado tete

Post Image

Dar es Salaam. Hali ya Mbunge wa Bunda Ester Bulaya aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH ) imeelezwa kuwa bado ni tete. Hali hiyo ni kufuatia tatizo la kupumua alilolipata baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu ya Kituo cha Kati cha Polisi mjini Tarime. Mwananchi lilifika katika wodi namba 18 Sewahaji alipolazwa mbunge huyo, lakini […]

Read More..

Mh. Ester Bulaya Kuletwa Muhimbili na Ndege

Post Image

Hali ya Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini Mh. Ester Amos Bulaya imezidi kuwa mbaya, kwa mujibu wa Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Mh. Joyce Sokombi, ambaye yuko naye hospitali akimuuguza. Mh. Sokombi amesema pamoja na kwamba amepelekwa katika hospitali ya mkoa Mara Mbunge huyo hajapata nafuu, hivyo amepewa rufaa ya kuja hospitali […]

Read More..

Mahakama yaamuru mke amuache mumewe kwa kut...

Post Image

Mahakama moja katika jimbo la Rajasthan nchini India imemuru mwanamke mmoja kuachana na mumewe wa ndoa, kwa sababu nyumba yao kukosa choo kwa muda mrefu. Jaji wa Mahakama ya Bhilwara, Rajendra Kumar Sharma, amesema kuwa kwa vile mume hakumjengea choo ndani ya nyumba, katika miaka mitano ya ndoa, basi huo ni ukatili wa kijinsia na […]

Read More..

Bulaya Sasa hamishiwa Bugando

Post Image

Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime alikokimbizwa Jana Jumapili baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu ya polisi mjini Tarime, amehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando jjijini Mwanza kwa matibabu zaidi.   Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche amesema kuhamishiwa Bugando kwa mbunge huyo kumewezekana […]

Read More..

VIDEO:Furaha Zatawala Mapokezi ya wanafunzi...

Post Image

Kilimanjaro. Furaha imetawala ujio wa watoto watatu wa Shule ya Lucky Vicent waliowasili leo Ijumaa, Agosti 18 wakitokea nchini Marekani kwenye matibabu baada ya kupata ajali Mei mwaka huu. Wazazi na ndugu waliruhusiwa kuingia ndani ya ndege hiyo kuwapokea watoto wao ambao wamepata nafuu kwa kiasi kikubwa. Wilson Tarimo alikuwa wa kwanza kushuka katika ndege […]

Read More..

Mke wa Mugabe akamatwa Afrika Kusini

Post Image

Johannesburg, Afrika Kusini. Grace Mugabe, ambaye ni mke wa Rais Robert Mugabe aweza awe amewafanyia ubabe watu kadhaa nchini kwake lakini kitendo cha kumshambulia, kwa waya wa umeme, mrembo mwenye umri wa miaka 20 kimemweka matatani. Mama Mugabe alikamatwa jana na alikuwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kwa kosa la kumshambulia mrembo huyo anayedaiwa kuwa ni […]

Read More..

Kashfa Zamrudisha Shigongo Darasani

Post Image

Mtunzi wa vitabu mashuhuri Tanzania Erick James Shigongo, anatarajia kurudi shule na kusoma elimu ya shahada, baada ya kuhangaika muda mrefu kutafuta nafasi hiyo, huku akisukumwa na masimango na matusi ya mitandaoni. Kwenye ukurasa wake wa facebook Erick Shigongo ameandika waraka mrefu akielezea safari yake kitaaluma na furaha aliyonayo, ya kuweza kufikia ndoto yake ya […]

Read More..

Waumini wakimbia Kanisa kupisha bomoabomoa

Post Image

Waumini wa Kanisa la Freedom Pentecostal Bible Tanzania lililopo Kibamba kwa Mangi wamelikimbia kanisa lao baada ya kukumbwa na bomoabomoa na jana, ibada ya Jumapili ilihudhuriwa na waumini 10 tu. Kanisa hilo ni miongoni mwa nyumba 30 za ibada zilizokumbwa na bomoabomoa hiyo ili kupisha upanuzi wa Barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kiluvya ikiwa […]

Read More..

Bill Gates Ajiunga Instagram Akiwa Tanzania...

Post Image

Dar es Salaam. Tajiri namba moja duniani Bill Gates amejiunga Instagram akiwa nchini Tanzania na kurusha picha tatu ikiwemo aliyopiga na watoto akiwa Muheza mkoani Tanga. Gates ameijunga na mtandao huo wa kijamiii kwa jina la thisisbillgates na kurusha picha zake za kwanza tatu zote akiwa Tanzania. Gates katika mtandao huo aliandika hiki, “Hello kutoka Tanzania, […]

Read More..

CUF Yapata Pigo Jingine

Post Image

Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kmepata pigo jingine kufuatia Mahakama Kuu nchini Tanzania kutupilia mbali pingamizi lao kutaka Profesa Ibrahim Lipumba asipewe ruzuku za chama hicho. Mahakama Kuu imetupilia mbali pingamizi hilo leo tarehe 11 Agosti 2017, kufuatia Chama Cha CUF huko nyuma kufungua kesi ya […]

Read More..