-->

Diamond Afungukia Ishu Yake ya Kuripoti Polisi

Msanii Diamond ameelezea kile kilitokea baada ya picha  kusambaa  zinazomwonyesha akihojiwa na jeshi la polisi.

Diamond akitoa maelezo mbele ya askari

Muimbaji huyo amedai alienda polisi kujieleza kwa jeshi la usalama barabarani baada ya jeshi hilo kudaka clip yake ya video inayomwonyesha aliendesha gari huku akiwa hajavaa mkanda.

Diamond na Kamanda Mpinga

Diamond ametoa taarifa hii kupitia ukurasa wake wa instagram

Leo nilireport kituo kikuu cha polisi wa usalama barabarani kutokana na Vidoe Clip tuliyopost naendesha gari barabarani bila kufunga mkanda na pia kuachia usukani na kucheza…. Nikapewa Onyo na Kulipa faini kulingana ya Mujibu wa sheria… tafadhali watanzania na Vijana wenzangu… tuhakikishe tunafunga mikanda pindi tupandapo na tuendeshapo Magari Maana ni Hatari kwa Maisha yetu na inaweza kukupeleka kunyea debe pia…?

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364