-->

Diamond, Msondo Patamu Hapo

MWIMBAJI wa Msondo Ngoma, Hassan Moshi William, amefafanua kilichowakera zaidi kwa Diamond Platnumz na kundi lake la WCB ni dharau ya kuwaita “zilipendwa” huku wakitumia kionjo chao bila ridhaa.

Katika moja ya posti alizozitupia kwenye ukurasa wake wa Facebook, Hassan ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mwimbaji na mtunzi tegemeo ndani ya Msondo Ngoma, marehemu Tx Moshi William, amesema wao (Msondo) hawakuhitaji pesa kama wengine wengi wanavyodhani, bali walihitaji sheria za kunakili kazi zifuatwe kwa wahusika.

“Wabongo bana, wakati wimbo “Zilipendwa” unatoka nilipokea simu nyingi sana, oooh.. utakuwa ushachukua chako wewe hawawezi kufanya tu hivi hivi, ndio haohao wanaichamba bendi, ooh.. mna njaa ninyi kwanza mmeshapotea Msondo wenyewe wamekufa, kwa sababu tu eti ni Diamond, dah jamani.”

“Waliopiga huo wimbo wote wapo na katika waimbaji aliyefariki ni mtunzi ambaye ni babangu Tx Moshi William, Maalim Gurumo na Joseph Maina tu,” ameandika Hassan.

“Kumbukeni hizo nyimbo zina hakimiliki, zinalipiwa kisheria na zimesajiliwa. Sasa mtu ooh.. alimpa gari Mzee Gurumo..?

Alimpa Gurumo kwa makubaliano yao binafsi na mapenzi yake hiyo haihusiani na kuchukua nyimbo ya bendi bila kuomba.”

“Alichokosea Diamond ni kuiita hii bendi “zilipendwa”, it means imepitwa na wakati wakati inaendelea kufanya kazi zake halafu unachukua vionjo vya hiyo hiyo uliyosema zilipendwa unatumia kwenye nyimbo yako ya kisasa,” alifafanua Hassan kwenye posti hiyo.

Hivi karibuni bendi maarufu nchini ya Msondo Ngoma iliteka vichwa vya habari baada ya mwanasheria wao kuiandikia barua WCB kudai fidia ya Sh300 milioni kwa kutumia kionjo cha wimbo wao wa “Ajali” bila ridhaa yao.

Wimbo wa “Ajali” ulitungwa na TX Moshi William miaka 12 iliyopita, mwaka mmoja kabla hajafariki dunia.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364