-->

Gabo Zigamba Ajinadi Kuikomboa Filamu

Muigizaji Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ amefunguka kwa kudai kwamba ameamua kujitolea kufa na kupona ili kunusuru tasnia ya filamu isonge mbele kwa kutumia Teknolojia ya simu  ambayo itawasaidia Watanzania kupata filamu bure na kwa urahisi.

Gabo amedai hayo wakati akizindua filamu yake ya ‘Kisogo’ kwamba ameamua kutoa sehemu ya maisha yake ili kuikomboa tasnia ya filamu ambayo imeonyesha kupoteza imani kwa mashabiki wa filamu nchini Tanzania kwa kutumia akili alizojaaliwa pamoja na kipaji chake kwa kadri atakavyopatiwa ushirikiano.

“Mimi nimeamua kuikomboa tasnia ya filamu. Haiwezekani nyimbo zinapata heshima kubwa kuliko filamu, wakati filamu  inaweza kuelezea kwa upana jambo na kueleweka. Unajua kuna wakati unafika lazima ukubali maneno ya watu ambao ni mashabiki wetu. Kwahiyo mimi binafsi nimeanza kutoa filamu fupi ambazo zitakuwa zikipatika katika App ya Uhondo, nimeanza na Kisogo, hizi filamu zimezingatia ubora ya kila kitu kuanzia picha, sauti, wahusika yaani kila ambacho kilikuwa kinazungumzwa mtandaoni kuhusu filamu,” alisema Gabo

Aliongeza,”Kwa sasa filamu fupi zitapatikana kupitia mtandao wa Uhondo na kila mtu mwenye simu ya mkononi ataweza kuzipata, sehemu ya 1 bure  na sehemu ya pili itakuwa ikichangiwa pesa kidogo ili kuweza kuzalisha kazi nyingi zaidi.  na kwamba malengo ya kufanya hivyo ni ili kila mtanzania aangalie filamu hizo na baadaye mambo yakikaa sawa zitakuwa zikipatikana bure kabisa
 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364