-->

Hashim Rungwe Ashikiliwa Polisi

Dar es Salaam. Aliyekuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Hashim Rungwe anashikiliwa na polisi kwa siku nne sasa.

Hashim Rungwe

Rungwe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Chaumma anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Mwanasiasa huyo anashikiliwa akituhumiwa kughushi nyaraka.

Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema leo Septemba 5 kuwa, Rungwe anashikiliwa kituoni hapo kwa siku nne.

Hata hivyo, Kamanda Mambosasa hakutaka kuingia kwa undani kuhusu suala hilo akisema hana taarifa za kutosha.

Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364