-->

Irene Paul: Sikuingia Kwenye Ndoa Kama Fasheni

UKITAJA waigizaji wanaojua nini wanapaswa kufanya mbele ya kamera na kuzitendea haki nafasi anazopewa kuigiza, basi huwezi kumuweka kando mwanadada Irene Paul, ambaye amecheza filamu nyingi, lakini msanii huyu alipotea kidogo baada ya kushika ujauzito ambao Mwenyezi Mungu amembariki na sasa ana mtoto wa kike, aliyempa jina la Wendo.

Irene Paul

 

Staa huyo amecheza filamu kama Love & Power, Kibajaji, Kalunde, Fikra Zangu, Penzi la Giza, I Hate My Birthday na nyingine kadhaa, wiki iliyopita alifanya mahojiano na Risasi Mchanganyiko nyumbani kwake Kigamboni jijini Dar na kufunguka mambo mengi kuhusu maisha yake ya kila siku.

Risasi Mchanganyiko: Mashabiki wamekumiss maana hawajakuona kwa muda mrefu sasa, vipi?

Irene Paul: Ni kweli lakini, nilipotea kidogo tangu nikiwa na ujauzito hadi nilipojifungua ndiyo maana wamenimisi, lakini wasijali najipanga na ‘soon’ wataniona tena.

Risasi Mchanganyiko: Mara nyingi suala la ujauzito wako linakuwa siri na hupendi kabisa watu wajue, hata wakati fulani ulishawahi kukana kama huna ujauzito mpaka ukatoa kiapo kikali, ni kwa nini inakuwa hivyo?

Irene Paul: Kwa kweli kama zamani ishu ya mimba nilikuwa naionea aibu sana, na kuichukulia tofauti na pia nilikuwa kama sikuwa na utayari wa kuitwa mama, lakini sasa hivi nimekua na hilo limeondoka kabisa.

Risasi Mchanganyiko: Hivi sasa kuna mtindo wa mastaa wajawazito kupiga picha na kujiachia sehemu kubwa ya miili yao, vipi wewe mbona picha zako hazijaonekana?

Irene Paul: Kwanza mimi siyo kwamba sijapiga picha kama hizo, ninazo lakini si za kuonekana kwa kila mtu, ni maalum kwa ajili ya mtoto wangu ajue kabisa wapi ametoka, na pia sisi tunaiga mastaa wa nje, wale wenzetu wanalipwa pesa ndefu, sisi tunajicho-resha.

Risasi Mchanganyiko: Mastaa wengi wana maisha ya kujifanya hawawezi kufanya kazi za nyumbani, vipi wewe kuhusu malezi ya mtoto?

Irene Paul: Yaani huwezi amini, mimi sina hata mdada wa kazi tangu nimezaa mtoto huyu namlea mwenyewe na ndicho nilichokuwa nataka kujifunza zaidi na kumjua mwanangu kiundani hivyo niko vizuri katika hilo.

Risasi Mchanganyiko: Hivi karibuni zilionekana picha kwenye mitandao umefunga ndoa lakini hakukuwa na staa hata mmoja aliyehudhuria na pia haikuwa na mashamsham, kwa nini?

Irene Paul: Sikuwaalika na pia nilifanya kitu kidogo, maana nia yetu tutakuja kuifanya sherehe tena baadaye na kila mtu atapata nafasi ya kuja kujumuika nasi.

Risasi Mchanganyiko: Mastaa wengi wakipata nafasi ya kuingia kwenye ndoa hawachukui muda wanaachika, wewe umejipangaje kuhusu hilo?

Irene Paul: Siwezi kusema nimejipanga, lakini ndoa ni kama mtihani, ni lazima usome kwa bidii ili ufaulu hivyo basi mimi sikuingia kwenye ndoa kama fasheni, nafaa kuwa mke bora kabisa, kwa nini nipewe nafasi ya kuwa mke halafu nifanye ushenzi.

Risasi Mchanganyiko: Kuna tetesi kuwa mumeo ni mume wa mtu pia, eti ndiyo maana humuweki hata kwenye mitandao ya kijamii, unalizungumziaje hilo?

Irene Paul: Kama angekuwa ni wa mtu si angejitokeza pale kanisani kupinga ndoa!

Risasi Mchanganyiko: Wanaume wengi hawapendi wake zao kujiingiza kwenye mambo ya sanaa wakiamini watapotea, vipi kwa upande wako hujakutana na hilo ‘biti’ kutoka kwa mumeo.

Irene Paul: Kwanza kabisa huwezi amini, tulijuana na mume wangu kabla sijawa msanii na hata nilivyojiingiza niko naye, na nilikuwa na wakati mgumu kumuhakikishia nitakuwa mke bora, nikiwa kwenye ndoa haitoingiliana na mambo yangu ya sanaa na ndivyo ninavyofanya.

Risasi Mchanganyiko: Nakushukuru sana Irene kwa ushirikiano wako.

Irene Paul: Asante karibu tena.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364