-->

Lady Jaydee Kumwaga Mipesa

Mwanamuziki mkongwe Lady Jaydee ameamua kumwaga fedha kwa mashabiki kupitia mitandao ya kijamii kwa kuanzisha shindano ambapo washindi watatu watakao weza kujibu kwa ufasaha maswali matatu atayatoa kwenye mitandao hiyo watalamba jumla ya milioni 2.

Lady Jaydee amesema katika mashindano hayo mshindi wa kwanza atajipatia milioni moja huku mshindi wa pili akipata laki saba na nusu na mshindi wa tatu atapata laki mbili na nusu ambapo kwa jumla atakuwa ametoa milioni mbili kwa washindi wote watatu.

Lady Jaydee ambaye sasa yupo katika kampeni ambayo baadhi ya mashabiki wake wamekuwa wakihisi huenda ni ujio mpya wa kazi yake mpya, huku wengine wakihisi huenda kuna jambo jingine mwanadada huyo anataka kufanya, lakini kwa mujibu wa historia Lady Jaydee amekuwa akifanya kampeni mara kadhaa pindi anapokuwa anaachia kazi zake za muziki.

Countdown na Lady Jaydee inakwenda kwa siku 20 ambapo ndipo washindi hao watapatikani lakini mpaka leo Septemba 5, 2017 zimeshapita siku siku 13 na kubaki siku saba kwa mantiki hiyo mshindi atapatikana mwanzoni mwa wiki ijayo.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364