-->

Madam Rita Afunguka Kuhusu Bongo Star Search (BSS)

MKURUGENZI wa Benchmark Production, Rita Paulsen, ametolea ufafanuzi kuhusiana na mchakato wa kusaka waimbaji chipukizi katika shindano lake maarufu la ‘Bongo Star Search’ linalofanyika kila mwaka.

MADAM RITA12

Rita Paulsen

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Rita kutambulisha kipindi chake kipya cha televisheni cha ‘Rita Paulsen Show’ kinachorushwa kila Jumapili katika runinga ya Azam two.

“Rita Paulsen Show ni kitu ambacho kimekuwa katika mawazo yangu zaidi ya miaka saba nyuma, kwa hiyo ni cha siku nyingi ni mipango ambayo nilikuwa nayo na sasa imetimia na ni moja tu ya mambo ambayo yapo pamoja na Bongo Star Search,” alisema.

Rita aliongeza kuwa, Bongo Star Search iko palepale na kuwatoa hofu Watanzania, huku akisema mazungumzo baina yake na uongozi wa Azam Tv yanaendelea kuona uwezekano wa kurusha matangazo ya kipindi hicho.

Kipindi cha Rita Paulsen Show ni kipindi cha kijamii chenye vipengele vya kuelimisha na kuburudisha familia.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364