-->

Majeruhi wa Lucky Vincent wazungumza kwa mara ya kwanza wakiwa wodini Marekani

Marekani. Madaktari wa Hospitali ya Mercy, ya Marekani wamesema watoto watatu majeruhi wa ajali ya Lucky Vincent, wanaendelea vyema.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameandika katika ukurasa wake wa faceboook kuwa watoto hao Saidia Ismael, Doreen Mshana na Wilson Tarimo watapelekwa katika makazi maalum ya kuangalia afya zao ikiwa ni pamoja na kupewa mazoezi ya viungo.

Pia watoto hao wameanza kuzungumza na kwa mara ya kwanza mtoto Saidia amesema ‘Helo Tanzania, na Wilson amesema ‘Thank you’.

“Ingawa wataendelea kuwa wodi ya watoto Mercy Hospital kwa sasa hadi madaktari bingwa watakapojiridhisha na hali yao,” ameandika Nyalandu

 Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364