-->

Mkojo wa Masogange Gumzo Mahakamani

MAHAKAMA ya Hakimu Mkasi Kisutu ilipokea ripoti ya uchunguzi wa sampuli ya mkojo ya Msanii Masogange kutoka kwa Mkemia Elias Mulima kwenda kwa ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kama kielelezo.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya mawakili wa Masogange, Nehemia Nkoko na Ruben Simwanza, kupinga mahakama isipokee ripoti hiyo ya uchunguzi ya sampuli ya mkojo kama kielelezo.

Baada ya kupokelewa kwa ripoti hiyo ya uchunguzi. Wakili Simwanza alimuuliza awali shahidi huyo kuwa ana uhakika huo mkojo ni wa Masogange?

Mulima akijibu swali hilo alidai kuwa ana uhakika sampuli ya mkojo aliyoifanyia uchunguzi ilikuwa ni ya Agnes.

Kwa upande wa shahidi mwingine wa upande wa mashtaka ambaye ni Ofisa wa Polisi kutoka ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum, WP Judith yeye alieleza jinsi alivyokabidhiwa Masogange, alivyompeleka kwa Mkemia na jinsi alivyotoa sampuli ya mkojo.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula kutoa ushahidi mbele ya Hakimu Wilbard Mashauri, WP Judith alidai kuwa siku hiyo alimpeleka hadi chooni, Masogange kutoa sampuli yake ya mkojo ambapo mshtakiwa aliingia chooni na yeye alikuwa nje na kwamba baada ya kutoka na sampuli ya mkojo, aliichukua na alikwenda kumkabidhi Koplo Sospeter.

Shahidi huyo alimtambua Agnes mahakamani hapo kwamba ndiye aliyekabidhiwa na kiongozi wake Naibu Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum, Ramadhan Kingai kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kufanyiwa uchunguzi.

Amedai alimpeleka Agnes katika ofisi hizo, Februari 15, 2017 kutokana na tuhuma za kutumia dawa za kulevya au kusafirisha.

Alidai alimchukua Agnes na aliambatana na Koplo Sospeter hadi kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kwamba walifika nyakati za saa saba mchana.

Alidai kuwa akiwa mapokezi alikabidhiwa chupa ndogo ya plastiki iliyokuwa na namba ya maabara 006/2017 na kuelekezwa ampeleke kwenye choo maalumu kwa ajili ya kutoa sampuli ya mkojo.

Shahidi huyo alidai kuwa aliondoka na mshtakiwa hadi chooni ambapo alitoa sampuli ambayo aliichukua na kumkabidhi Koplo Sospeter.

Wakili wa Masogange, Ruben Simwanza. alimhoji shahidi huyo kuwa ulikabidhiwa kumpeleka mshtakiwa kwa Mkemia alitoa mkojo wa rangi gani?

WP Judith: ulikuwa na rangi ya njano iliyopauka.

Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka Alhamisi wiki hii.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364