-->

Mr Aomba ieleweke Kuwa Hana Ugomvi na Diamond

Mr Blue amesema hana tatizo na Diamond Plutnumz licha ya hivi karibuni kuibuka sintofahamu katika mitandao ya kijamii juu ya nani mmiliki halali wa jina ‘Simba.’

mr blue342

 

Blue ambaye anajipanga kuachia wimbo mpya akiwa na Alikiba mwezi huu, amekiambia kipindi cha The Weekend Chart Show cha Clouds TV kuwa aliamua kuweka wazi kwa umma juu ya umiliki ya jina hilo kama namna ya kusherehekea mafanikio baada ya wasanii kadhaa kumuiga.

“Kile kitu hakikuwa drama au ugomvi na mtu mimi nilifanya kama kujipongeza, kwa sababu kama wewe ni shabiki yangu na unanifuatilia vizuri kipindi cha nyuma nilikuwa napost simba na slogan yangu ‘Simba kaamka na njaa kali’ yaani baada ya kukaa muda mrefu bila ngoma nilivyokuja kutoa ‘Pesa’ nikaandika Simba kaamka na njaa kali,” alisema.

Aliongeza, “Pia nilitumia jina Simba kutokana kuwa na sauti ya kukwaruza kwenye muziki wangu. Sasa siku zinavyokwenda nikaona baadhi ya wasanii wengi tu sio Diamond wengine wapo Mwananyamala huko,Kigogo wanatumia jina la Simba. Ikanipa moyo kwamba kitu ambacho nimekigundua watu wamekikubali.

“Kwahiyo nikapost kitu kwa kujipongeza kwa kitu nilichokigundua miaka 2/3 nyuma leo kila mtu anataka kutumia. Lakini sasa mashabiki wanaichukulia vibaya kwa sababu ana mashabiki wengi, angechukua mtu ambaye yupo chini yangu nadhani yasingetokea haya, kwahiyo naomba ieleweke mimi sina ugomvi na Diamond na sijawahi kuwa na ugomvi na Diamond.”

Chanzo: Bongo5

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364