-->

Mwigizaji wa TMT Aula Rwanda

MWIGIZAJI chipukizi Shiraz Ngasa aliyeibuliwa na shindano la kusaka vipaji vya filamu kupitia Tanzania Movie Talent (TMT) amefanikiwa kuigiza filamu kubwa nchini Rwanda kama muigizaji kinara na kufanya vizuri kwa kumwagiwa sifa lukuki kulingana na kipaji alichoonyesha.

Shiraz akiwa katika pozi la picha.

“Rwanda wamejipanga katika ujio wao wa utengenezaji filamu haikuwa rahisi kupata nafasi ya kuigiza katika filamu ya Seeds of memory kama mhusika mkuu (Steringi) nimeitanga Tanzania,”alisema Shiraz

Shiraz akiwa katika moja ya scene akicheza filamu kubwa Rwanda.

Msanii huyo ambaye alifanikiwa kuchaguliwa baada ya usaili mkubwa kufanywa nchini Rwanda anasema kuwa amezidi kukua zaidi kwani kwa mara ya kwanza amekutana na waongozaji wa filamu kutoka Hollywood wamemjenga zaidi, sinema ya Seeds of Memory imeshirikisha nyota wa Afrika ya mashariki.

Shirazi akiwa ndani ya scene ya hisia katika filamu hiyo

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364