-->

Mzimu wa Kanumba wamsumbua Ray Kigosi

Ikiwa ni zaidi ya miaka minee toka alipofariki dunia msanii wa filamu nchini Kanumba The Great lakini bado wapenzi wa filamu nchini na mashabiki wanaonesha kukubali zaidi kazi zake.

ray562

Hali hiyo imepelekea wapenzi kusema kuwa aliyekuwa mpinzani wake katika tasnia hiyo Ray Kigosi ameshindwa kufikia kiwango ambacho alikiacha Kanumba miaka minne nyuma.

Leo kupitia ukurasa wa Facebook wa Eatv tuliweka post ambayo inauliza kama kuna mtu katika tasnia ya filamu ameweza kufikia kiwango alichofikia Marehemu Kanumba kabla ya kifo chake na ndipo hapo mashabiki walipoanza kusema walikuwa wanategemea kuwa Ray Kigosi ndiye ambaye angeweza kufikia kiwango hicho lakini wanasikitika kuona msanii huyo ameshindwa kufikia matarajio yake.

Hivyo ni wazi kuwa Mzimu wa Kanumba bado unamsumbua Ray Kigosi kwani mashabiki bado wanashindanisha kazi za sasa za Ray na zile alizofanya marehemu Kanumba enzi za uhai wake na wanadai kuwa kazi za Kanumba bado ni bora zaidi ya kazi anazofanya Ray Kigosi sasa.

Haya ni maoni ya baadhi ya mashabiki katika ukurasa wa facebook wa EATV ambao wameonesha ni jinsi gani Kanumba The Great alikuwa ni mtu wa tofauti kwao katika kazi zake ukitofautisha na wasanii wa sasa akiwemo aliyekuwa mshindani wake mkubwa kipindi hicho Ray Kigosi

Johannes Patrick Nyabara: For sure mpaka sasa sijamuona wakumfikia marehemu Kanumba, nilitegemea Ray Kigosi angefanya hivyo kumbe I was Wrong. Marehemu Kanumba pumzika kwa amani, umeacha pengo lisilozibika kabisa katika tasnia ya filamu. Namshangaa sana Ray Kigosi alikua vizuri baada ya kutengana na Kanumba mambo yakawa kinyume, sasa amebaki kujichubua tuu” Alisema Nyabara

“Kitu ambacho nimekigundua baada ya Steven Kanumba kufariki ni kwamba Ray alikuwa akicopy na kupest filamu za Kanumba ndio maana leo hii Ray kapotea kwa sababu aliyekuwa anamcopy amefariki, mtakumbuka kipindi kile Kanumba akitoa filamu na Ray anatoa na Ray aliwahi kukiri hilo alipoulizwa na gazeti moja alikiri kwamba kifo cha Kanumba kimemshusha kisanaa” Alisema Alphonce Sekwao

“sijawahi kununua move ya Ray hata moja. Kwanza akiigiza unaona kabisa anasoma maneno mdomoni kwake. Miaka mia hatomfikia wala hawatomfikia marehem Kanumba.” Alidai Fatuma Salum

“Kwakuwa sasa ufuatiliaji wa movie umekuwa mdogo, mpaka sasa sijui ni movie gani mpya imetoka, alihamasisha sana watanzania na hata nchi za jirani kupenda kuangalia sio za kwake pekee bali uwepo wake ulionyesha hata wengine tuliokuwa hatuwafamu, kwasasa hatujui ma upcoming wengine kwenye bongo movie hata wale waliosikika kipindi yupo Kanumba wanaonekana kama wameachana na sanaa kabisa,pengine tusubiri baadae sana na sijui wanaokuja wataigiza nini, hakuna mfano wa kuigwa bongo movie chali. Alisema Sichinga William

“Mnajua Steven Kanumba The Great alikuwa na uthubutu na kujiamini, sio kwamba kabla yake kulikuwa hakuna filamu , filamu zilikuwepo lakini zilikuwa ni filamu za kimazoea tu na wasanii wa zamani waliamini hawawezi kuwafikia waigizaji wa Nigeria au Ghana lakini Kanumba The Great alikuja kuleta mapinduzi na ushindani wa hali ya juu aliamini kwani wao Nigeria na Ghana waweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini? aliuliza Alphonce Sekwao

“Kwasasa hakuna lakini atakuja patikana tu, kwan hata yeye hakujua kama angefika huko alianzia chini na akajituma sana katika sanaa ndio alifika hapo alipofika,sema kwa waliokuwepo sasa watasubiri sana Kanumba alikuwa anajua sana, lakini huko mbele tutapata tu mrithi wake, hakuna linaloshindikana chini ya jua.” Alisema Yousuph Bayagubu.

Comment

Chanzo: EATV.TV

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364