-->

Nay wa Mitego Anakula Madawa – Niva Super Mario

Msanii wa filamu nchini Niva Super Mario ameendelea kumsakama Nay wa Mitego kwa kusema kuwa msanii huyo hana nguvu na si mtu wa mazoezi bali ni mtu ambaye anakula madawa ya kuongeza nguvu na mwili huku akitafuta kiki kupitia bongo movie.

Niva alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) na kusema hiyo ndiyo sababu kubwa msanii huyo amekuwa anakimbia mapambano kila anapoombwa wazipange , lakini pia Niva anasema Nay wa Mitego anatafuta kiki kupitia bongo movie.

Nay anapokuwa anaingia studio au kutoa wimbo mpya ndiyo amekuwa akiichokoza bongo movie ili apate kiki, Nay ni mtu ambaye hana heshima halafu kwa wachache wanaomuogopa ndiyo wanatia kiburi labda vile vijitu vyake anavyovimiliki sijui producer, meneja ndiyo wanamtia kiburi. Sisi huku bongo movie tunafanya kazi kubwa zaidi yake yeye. Mimi Nay wa Mitego namjua nguvu yule hana, Nay hana mazoezi ule mwili anakula madude  (madawa) yao ya kukuza mwili, Nay hana mazoezi mimi ndiyo namjua Emma Chogo”  Alisisitiza Niva Super Mario

Mbali na hilo Niva anasema wao waliandamana kwa lengo kuimbia serikali kuwa kuna watu hawalipi kodi kama wao wanavyolipa lakini pia alisisitiza kuwa katika nchi za Afrika Mashariki wameshafanya sana kazi ya kuwafurahisha watu kwa kazi zao sasa umefika wakati na wao waanze kunufaika na kazi zao za sanaa.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364