-->

Nililipwa Elfu 50 Kwenye Filamu Yangu ya Kwanza-Nisha

Msanii wa filamu na mjasiriamali, Salma Jabu aka Nisha amesema licha ya sasa hivi kumiliki kampuni yake ya filamu, pesa yake ya kwanza kulipwa katika filamu ilikuwa ni shilingi 50,000.

Nisha

Nisha ambaye kwa sasa ni miongoni mwa wasanii wenye mafanikio kwenye filamu, amekiambia kipindi cha Uhondo cha EFM kuwa baada ya kuanza kupata mafanikio kidogo kidogo kwenye filamu aliwekeza na kununua vifaa pamoja na kuanzisha kampuni yake.

“Filamu yangu ya kwanza kulipwa nililipwa elfu 50, pesa niliyoitumia kuwekeza hadi leo namiliki kampuni yangu,” alisema Nisha.

Pia Nisha alisema baada ya kupata jina katika filamu na kuanza kupata pesa, alijiingiza pia katika biashara kubwa za nguo ambazo amedai zinamnufaisha zaidi mpaka sasa.

Kwa sasa Nisha anajipanga kuachia filamu mpya ‘Kiboko Kabisa’ iliyotayarishwa chini ya kampuni yake, Nisha’s Film Production.

Bongo 5

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364