-->

Ray C Afungukia Swala la Mahusiano Yake Kwasasa

Msanii Rehema Chalamila a.k.a Ray C ambaye ametamba kwenye anga la Bongo Fleva kwa siku nyingi, ameweka wazi kuwa kwa sasa hayuko kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote.

Ray C ambaye amerejea kwenye game kwa kasi baada ya kutoka kwenye dimbwi ya matumizi ya dawa la kulevya, amefunguka hilo alipokuwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV, na hakutaka kueleza sababu za kuamua kuishi bila mpenzi.
Msanii huyo aliyewahi kutikisa na ngoma kadhaa za bongo fleva zenye ujumbe wa mahaba kama vile Wanifuatia nini, Na wewe milele n.k atatikisa jukwaa la Azura Jumanne katika usiku wa Valentine, ambapo amesema amepania kutoa burudani kali kutokana na kukaa muda mrefu bila kufanya show,

Ameahidi kukata kiu ya wote waliokuwa wamem-miss huku akiwataka kufika ukumbini hapo na wapenzi wao “Mimi ni mtu wa mapenzi, nimetayarisha nyimbo nzuri, sijafanya show muda mrefu, nitaimba nyimbo zangu kadhaa, na nawashauri kila mtu aje na mpenzi wake, ndiyo Valentine itanoga, pia kutakuwa na kila aina ya burudani pamoja na dinner”

Kuhusu kurudi, amesema ana hamu ya kurudi kwenye game na tayari amesharekodi nyimbo kadhaa, lakini alishauriwa aanze na Valentine kwanza

“Naendelea kurekodi, bosi wangu alinishauri nifanye kwanza kwa ajili ya Valentine maana watu wanaulizia sana”

KUHUSU RECHO
Katika hatua nyingine, Ray C alitakiwa kutoa maoni yake kuhusu Msanii Recho ambaye amekuwa akifuata nyayo zake kuhusu kutajwa kwake kwenye orodha ya watu wanaohusika na dawa za kulevya, lakini alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hana uhakika juu ya suala hilo

“Mimi Recho namjua vizuri, lakini kutokana na matatizo yangu sijaonana naye muda mrefu sana, sipo hapa kumzunguzia mtu, na siyo vizuri, pia siyo vizuri kuzungumzia kitu ambacho sina uhakika nacho maana mimi sijawahi kumuona akitumia hiyo kitu. Nachoweza kusema ni kuwa kama mimi niliweza, kila mtu anaweza, naamini atakuwa poa maana najua ni mwanamke imara” Amesema Ray C

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364