-->

TCRA Yazungumzia Jinsi ya Kuhama Mtandao wa Simu

Dar es Salaam.Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) imezindua mpango wa elimu kwa umma kuhusu hudumu ya kuhama mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani (MNP).

Akizindua mpango huo leo Jumatano asubuhi, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema lengo ni kuwapa uhuru wateja kutumia mtandao bora zaidi, pia kuongeza ushindani kwa watoa huduma na kuboresha huduma zao.

Kilaba amesema mabadiliko hayo ni mwendelezo wa maendeleo ya teknolojia nchini ukizingatia kwamba watumiaji wa simu wameongezeka kutoka milioni 2.9 mwaka 2005 mpaka kufikia milioni 40.1 Disemba, 2016.

“Uanzishwaji wa MNP ni kwa mujibu wa kanuni za mwaka 2011. Kanuni hizi zinawataka watoa huduma za simu za kiganjani kuwezesha huduma hii katika mitandao yao.”

By Peter Elias, Mwananchi

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364