-->

Tunda Afunguka Kuhusu Maisha Yake Baada ya Kutajwa Sakata la ‘Unga’

Mrembo  maarufu aliyependezesha video ya ‘Furaha’ ya Young D, Tunda 76 amedai kutajwa kwake kwenye orodha ya wanaohusika na dawa za kulevya kumempa changamoto ya kuaminika nyumbani kwa wazazi wake.

 

Tunda amezungumza hayo leo kwenye eNewz ya EATV na kusema kuwa tangu kutajwa kwenye wahusika wa matumizi ya madawa imemfanya kubadilisha mpaka mfumo wa maisha kwa kuwa nyumbani kwa wazazi wake wamekuwa wagumu kumuelewa.

“Nimebadilisha mfumo wa maisha, naishi maisha ya low profile kwa sasa ili mambo kwanza yatulie lakini nipo. maisha ya mitandaoni nimeacha. Suala la kutajwa linaniumiza kwa sababu nyumbani haikuwa rahisi kueleweka na wazazi. Viongozi wanadai natumia mimi ndo niseme najitetea ukweli ni vigumu mno lakini naamini kwenye ukweli uongo hujitenga pembeni ipo siku ukweli utajulikana na maisha yataendelea kama kawaida. Niweke wazi situmii madawa ya kulevya”. Alisema Tunda

Tunda na baadhi ya mastaa wengine wapo nje kwa dhamana baada ya kutuhumiwa kuhusika na matumizi ya madawa ya kulevya.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364