-->

Ushuru Wamkwamisha Baby Madaha Kuingiza Nchini Vifaa Vyake vya Filamu

Ushuru mkubwa unaotozwa katika bandari ya Dar es Salaam, umemzuia Baby Madaha kuingiza vifaa vyake vya filamu alivyovinunua mwaka jana mjini Dubai.

Baby Madaha

Baby Madaha

Muimbaji na muigizaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa serikali ya awamu ya tano imeongeza ushuru kiasi cha kuharibu mipango ya watu wengi. Amedai kuwa vifaa hivyo bado vipo Dubai alikohamishia makazi yake.

“Nilileta baadhi ya vitu lakini nikawa natakiwa nilipe nusu ya price ambayo nimenunulia. Kwa mfano ile mashine ya dubbing, nimenunua milioni 20 kwahiyo nusu yake ni milioni 10 ninaitoa wapi kama msanii tu wa kawaida? amehoji Madaha.

Muimbaji huyo amesema anachosuburia kwa sasa ni kuangalia kama kweli serikali imepanga kuondoa ushuru kwa wasanii kwakuwa wataanza kutozwa kodi.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364