-->

Wanaume Vinara wa Michepuko – Kigwangalla

Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefunguka na kusema kuwa wanaume wengi wamekuwa vinara wa michepuko jambo ambalo linapelekea kupata virus vya UKIMWI na kwenda kuwaambukiza wanawake.

Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.

Kigwangalla amesema hayo leo bungeni wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti maalum CHADEMA, Susan Lyimo ambaye alitaka kujua kwanini idadi kubwa ya wanawake ndiyo wamekuwa waathirika wa virus vya UKIMWI, akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Afya alikiri kuwa ni kweli kuna utofauti japo si mkubwa sana na kudai kuwa wanawake wengi wanapata maambukizi haya kutokana na utofauti wa kibaolojia wa maumbile lakini pia kutokana na mienendo ya wanawake na wanaume.

“Maambukizi kati ya wanawake na wanaume kuna uwiano, lakini hili la wanawake kuwa wengi kuonekana wanapata virus vya UKIMWI ni kutokana na utofauti ya kimaumbile ya kibaolojia kati ya wanawake na wanaume, tabia za wanaume na wanawake. Lakini wanaume wengi wamekuwa na tabia za kuchepuka sana hivyo wao wanaweza kuvitoa virus huko na kuleta kwa wamama nyumbani, maana wanaume ndiyo chanzo cha michepuko ukilinganisha na wanawake” alisema Kigwangalla

Mbali na hilo Kigwangalla aliwataka wanaume kuachana na tabia za michepuko, na kujiwekea utaratibu wa kupima afya zao na wenza wao ili wame na uhakika na afya zao na kutopeleka virus hivyo kwa wake zao majumbani kwao.

“Mimi nawashauri wanaume waepukane na michepuko watulie kwenye ndoa zao, tujiwekee utaratibu wa kupima hali zetu na wenza wetu, kwa wale ndugu zangu waislam tumepewa fursa ya kuoa hata wake nne, hivyo ni bora upime hali za wenza wako wote hao kisha uoe wote na kuepukana na michepuko tunayoiokota huko, ni bora upime ili uchukue mtu na kuweka ndani kabisa” alisisitiza Kigangwalla

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364