-->

Aunt Ezekiel: Achana na Mimi Wewe Wema Sepetu

MASTAA wawili waliokuwa mashosti siku za nyuma, Aunty Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’ wameingia kwenye msuguano tena hivi karibuni huku hali ikionesha kuwa mastaa hao kwa sasa ndiyo basi tena.
wema sepetu899
Hali hiyo imetokea juzi baada ya Aunty kuweka picha ya kumtakia siku njema ya kuzaliwa rafiki na msanii mwenzake, Maimartha Jesse kwa kuandika, “Happy bday Kipenzi cha Roho yangu …..Unajua kama Nakupenda cha zaidi Naomba Yesu Akutunze milele.”
Katika post hiyo, followers kadhaa wa Aunty walikomenti akiwemo staa mwenzake kwenye tasnia hiyo, Wema Sepetu aliyekomenti Yesu atamtunza…Baada ya hapo, Aunty akaibuka na kumtolea povu Wema akimchana Achana na mm ww @wemasepetu“ hali iliyoibua maswali na mijadala mingi mitandaoni, huku watu wakitaka kujua kwa nini Aunty amemshushua hivyo Wema.
wema-sepetu-na-aunty
Inasemekana kwamba, chanzo ni Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, Wema kumsema vibaya Aunty kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram. Kwa hali ilivyofikia mpaka sasa inaonesha sio rahisi tena kwa waigizaji hao kuelewana.
Tangu siku za hivi karibuni, Wema alipokosana na rafiki yake Muna Love na kumsema vibaya kwa kutumia video aliyojirekodi na kuisambaza mitandaoni, Wema kwa sasa amekuwa akijitahidi kuwa karibu na Aunty ili warudishe urafiki wao wa zamani japokuwa jitihada zake zinaonesha kugonga mwamba baada kuambulia maneno mazito kutoka kwa Mama Cookie.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364