-->

Aunt Ezekiel Awajibu Wanaodai Anajipendekeza kwa Zari

Malkia wa filamu na mama wa mtoto mmoja, Aunt Ezekiel amewamind mashabiki katika mitandao ya kijamii ambao wanadai anajipendekeza kwa mama watoto wa Diamond, Zari, baada ya hivi karibuni kuonekana akila nao bata pamoja.

zari022

Mwingizaji huyo ambaye alikuwa rafiki wa Wema Sepetu, amesema lazima awe karibu na familia ya bosi wa mume wake kwa kuwa hao ndio waliomwajiri mume wake.

“Nataka niwaambie kitu kimoja maana kujibu mmoja mmoja muda huo sina ni hivi nafanya nitakalo sifanyi mtakayo, maana nina uhakika nyie mnaokaa kubishana na mimi vibanda vya mbavu za mbwa vinawashinda, so muda mnaokaa mkafatilia yangu mngeenda kutafuta yakufanya, ooh! njaa yes i say tena yes maana mnataka nibadili red kuwa yellow kwani yule si ni boss wa mkata viuno wangu au!. Sasa kama ni bosi ulitaka nibishe niseme mimi ndio bosi, basi nifungue bendi yetu acheze!,” Aunt Ezekiel aliandika instagram.

Aliongeza, “Mnawazimu nini na namweshimu kama mshkaji rafiki bosi wa bwana yangu na siwezi acha kushirikiana na familia yake eti kisa ushuzi mtasema nini. Sitaki kutaja majina ya watu ila kilichopo ndio ukweli asilia, Mama Tee ndio mwanamke na mama watoto wa Nasibu no way hata tulambe lami kubadili ni ngumu ila mwenyewe akibadili basi na sisi tutabadili ila kwa sasa ni Mama tee shukrani gud Day,”.

Mwigizaji huyo anatoka kimapenzi na densa wa Diamond, Mose Iyobo ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kupata mtoto mmoja aitwae Cookie.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364