-->

‘Baba yake Diamond: Nililia sana kutoalikwa kwenye arobaini ya Tiffah’

Baba wa staa wa muziki Diamond Platnumz, Abdul Juma amesema hakuna siku alilia kwa uchungu kama siku ambayo mjukuu wake Tiffah alifanyiwa sherehe ya arobaini bila yeye kualikwa.
Diamond na Baba Yke

Akizungumza katika kipindi cha The Weekend Chat Show cha Clouds TV Jumamosi hii, Mzee Abdul alidai licha ya kuwa anawasiliana mara kwa mara na mama yake Diamond, lakini hakuwai kupewa taarifa yoyote kuhusu tukio hilo mpaka alivyoona picha kwenye magazeti.

“Hakuna kitu kiliniuma kama kufanyiwa shughuli kwa yule dogo bila kualikwa.” Alisema Mzee Abdul.

“Yaani nakumbuka nilipigiwa simu nikaambiwa baba mwanao amepata mtoto lakini sio siku ya arobaini, niliumia sana, nililia, nililia sana kutoalikwa kwenye arobaini. Mimi nachoomba (Mama Diamond) asinisahau, kuna kazi nilifanya mpaka akawa hapo,” aliongeza.

Katika hatua nyingine mzee huyo amemtaka Diamond kufanya kazi kwa bidii.

“Mimi nampenda sana, kama kuna baya niliwatendea wanisamehe, mzazi akosehi, pia aendelee kujituma zaidi,” alisema Mzee Abdul.

Bongo5

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364