-->

Chege Kuvunjika TMK Wanaume, Mh Jakaya Alihuzunika

Msanii kutoka kundi la Wanaume Family, Chege Chingunda amefunguka na kusema kuvunjika kwa kundi la ‘Wanaume TMK Familiy’ kulimuuzunisha mpaka aliyekuwa Rais wa awamu ya nne ya Tanzania Mh. Jakaya Kikwete.

Msanii Chege akisalimiana na rais wa awamu ya tano, Dkt Jakaya Kikwete. (PICHA:MAKTABA)

Msanii Chege akisalimiana na Rais wa awamu ya tano, Dkt Jakaya Kikwete.
(PICHA:MAKTABA)

Akizungumza kwenye kipindi cha MKASI kinachorushwa na EATV Chege alisema kuwa Rais Kikwete aliwaambia kuwa amehuzunishwa sana na kitendo cha kundi hilo kuvunjika kwani alikuwa akiona jinsi ambavyo walikuwa wamefanikiwa kuteka nchi kwa burudani na vile ambavyo waliweza kutoa burudani ya nguvu na kufanya biashara ya nguo zao na jinsi wananchi walivyokuwa wakiwapa support.

Chege amedai hata yeye mpaka sasa anatamani sana kundi hilo liweze kurudi kama lilivyokuwa awali, kwani kuna vitu vingi ambavyo anavikumbuka vilikuwa vinafanyika enzi hizo.

“Kiukweli kabisa mimi mwenyewe na kila mtu anatamani kundi la TMK Wanaume Familiy lirudi kama zamani hata sasa, sababu kuna vitu tulikuwa tukifanya navikumbuka sana, na siamini kama kuna mtu ndani ya kundi lile ambaye hapendi hicho kitu kitokee. Kuna wakati mpaka tuliitwa na Rais Jakaya Kikwete ili aweze kutuweka sawa turudi kama zamani sema mwenzetu mmoja hakuweza kutokea” Alisema Chege.

“Kuna wakati tulikuwa tunaweza kupanda stejini ili show iweze kuisha lazima polisi waingilie kati, na kuna siku zingine kwa siku moja tulikuwa tunaweza kufanya mpaka show tatu sehemu tofauti tofauti yaani hapo tunabadili nguo tu na kupanda sehemu nyingine, kiukweli nakumbuka mambo kama hayo” Aliongeza Chege.

Mbali na hilo Chege anakiri wazi kuwa msanii Juma Nature na uongozi ndiyo walikuwa na tatizo lao ila yeye si chanzo cha kundi hilo kuvunjika kama ambavyo baadhi ya watu wanavyodai kuwa mwanamke ndiye alikuwa chanzo kwa kundi hilo kuvunjika. Lakini mbali na hilo Chege pia amekiri kuwa Juma Nature ndiye alikuwa msanii mkubwa kwenye kundi hilo na yeye aliweze kuwaweka wao kwenye ramani ya muziki wa bongo fleva mpaka kufikia hatua ya kufanya vyema na kukubarika kwa jamii.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364