-->

Hivi Ndiyo Alikiba Alivyochukizwa na tetesi za Abdul Kiba kujiunga WCB

Miezi michache iliyopita Abdul Kiba ambaye ni mdogo wake na AliKiba alinukuliwa vibaya na vyombo vya habari kwamba yupo tayari kujiunga na label ya ‘WCB’ ya Diamond kauli ambayo ilileta shida kwa mashabiki wa AliKiba pamoja na team yake.

kiba34

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘Bayoyo’ ameiambia Bongo5 kuwa kauli hiyo ilimfanya aonekane msaliti.

“AliKiba alijisikia vibaya kwa sababu alijua kama ndo vile tena ndugu yake nimekuwa msaliti kumbe ni watu walipata definition nyingine na ni kitu ambacho hakiwezekani ila niliweza kufanya interviews nikaweka mambo sawa,” alisema Abdul Kiba.

Akifafanua kauli yake aliyozungumza na kutafsiriwa vibaya Abdul Kiba alisema “Siku ambayo nilifanya interview walinielewa vibaya maongezi yangu, unajua unaposikia kwamba kuna kazi hakuna kazi ya bure, kazi yoyote lazima iwe na malipo, nilikubali kwamba kama WCB watanihitaji kwa kolabo au show naweza nikajoin nao kufanya kazi ila sikutoa kauli kwamba naweza kwenda label yao kwa sababu hata mimi na label yangu,”

Pia muimbaji huyo amewashukuru mashabiki wa team Kiba kwa kuendelea kuwasapoti wasanii wake pamoja na kazi zao.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364