-->

Kutoka Maisha Plus Babu Aahidi Tukio Kubwa

WAKATI washiriki 29 wa Maisha Plus East Afrika 2016 wakiwa tayari kambini kwa safari ya kuisaka Sh milioni 30 itakayotolewa kwa mshindi mmoja tayari mambo mbalimbali yamepangwa kufanyika.

Babu wa kijiji hicho cha Maisha Plus

Babu wa kijiji hicho cha Maisha Plus

Babu wa kijiji hicho cha Maisha Plus ambaye ndiye mwenyeji wa kijiji hicho ameweka wazi kwamba kuna tukio kubwa litakalofanywa katika kijiji hicho ambalo halikuwahi kutokea huku akificha siku ya tukio hilo kufanyika.

“Nawataka mashabiki wa Maisha Plus wawe wanaendelea kuangalia Kijiji cha Maisha Plus kupitia Azam Two kwa kuwa kuna tukio kubwa ambalo halijawahi kutokea litatokea hivi karibuni hapa hapa kijijini, lakini siweki wazi ni lini hivyo muendelee kuangalia,” alieleza Babu Rajabu.

Kwa sasa washiriki wametakiwa kujenga nyumba zao za kuishi huku wakitumia maji ya kununua na kiasi cha Sh 4,000 walizopewa na hazitakiwi kuisha kabla nyumba wanayojenga haijaisha.

Licha ya kuishi kwa muda mfupi, lakini baadhi ya washiriki wameshaanza kuonyesha makali yao na kujuana tabia huku lugha ya Kiswahili na Kiingereza ikitawala. Pia wapo wale mabingwa wa kupiga kimya na huwa wakiishi muda mrefu kwa kuwa hawajulikani majina yao na wengi hivyo huwa hawatajwi katika kikaango.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364