-->

Maneno ya Jay Moe Kwa Wasanii Wakongwe

Jay Mo amesema baada ya kutoa ngoma yake ya ‘Pesa Madafu’ amengundua mengi yakiwemo mabadiliko ya music wa kisasa huku akisema kipindi chao ilikuwa lazima utoe albamu ndo uuze lakini kwa sasa mtu anasingle mbili anasifa.

JAYMOE

Jay Moe

Mkongwe wa muziki wa rap ambaye alikaa kimya kwa miaka 11 kwenye gemu na kuibuka na ngoma kali inayosumba mitaa PESA MADAFU, Namzungumzia Jay Mo amewatahadharicha wakongwe kuwa gemu kuwa ‘limechange so’ kama wana rudi kimuziki na wanataka kuhit inabidi wajue na swag za kinyamwezi zinazotrend kwa sasa.

Jay Mo anasema msanii mzuri ni yule anayeweza kubadilika na mazingira yanavyokwenda na kuweza kubadilika na nyakati zinavyokwenda ili kuendelea kukalia nafasi zao walizokuwa nazo tangu zamani ila wakirudi na staili zao za zamani watashindwa kukimbizana na gemu.

Hata hivyo Mo aliiambia eNewz kuwa hashauri wanamuziki chipukizi kuamini kwamba hata ukifanya muziki muzuri ukafanya video zuri utatoka kimuziki kwa kuwa huwa nyimbo nyingi zinzobebwa na video hutoka na kupotea kwa muda mfupi sana.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364