Mimi Siyo Chizi, Wao Ndiyo Wazinguaji – Ruby
Msanii wa Bongo Fleva Ruby ambaye leo ameachia kazi yake mpya inayofahamika kwa jina la ‘Wale Wale’ ambayo imetayarishwa na mtayarishaji Man Water amefunguka na kusema kuwa yeye siyo chizi kusema ashindwe kutokea kwenye baadhi ya video ya wasanii.
Ruby akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo amesema kuwa alikuwa hana haja ya kukataa kuonekana kwenye baadhi ya nyimbo ambazo yeye ameshirikishwa ila kuna wakati mwingine watu hao walikuwa wakimzingua.
“Unajua ukisikiliza maneno ya upande mmoja unaweza kudhani labda kinachoendelea ni sawa mimi siwezi kukataa kufanya video zao sema muda mwingine unakuta wao ndiyo wanazingua, kuna muda mwingine mimi ndiyo nazinguliwa, watu wananikwamisha ili nisionekane kwenye hizo video” alisema Ruby
Mbali na hilo Ruby amewataka mashabiki zake wasahau mambo yoyote yaliyotokea kipindi cha nyuma na sasa amekuja kivingine na anaomba support kwa mashabiki.