Navy Kenzo: Tukigombana Ndiyo Tunatoa Wimbo Mzuri
WACHUMBA wanaounda kundi la Navy Kenzo, Aika Mareale na Nahreel, wamesema wanapogombana ndiyo hupata nafasi ya kuandika wimbo mzuri.
Akizungumza na MTANZANIA, Aika alisema hatua waliyopiga kimuziki na kimapenzi ndiyo inayowapatanisha kwa muda mfupi wanapogombana.
“Huwezi amini huwa tunagombana sana na mpenzi wangu na wakati mwingine tunafikia hadi hatua ya kutaka kuachana, lakini tukifikiria tulivyo kimuziki na namna tulivyohangaika kuitafuta Navy Kenzo kila mmoja hujikuta akimrudia mwenzake na kuongeza upendo.
“Na huwa kila tunapopatana baada ya kugombana sana tunatunga wimbo unaoshika mashabiki na kututangaza vyema kitaifa na kimataifa kwa ujumla,” alieleza Aika.
Mtanzania