-->

Nyumba ya Gwajima Yapigwa Picha

Dar es Salaam. Wakili Peter Kibatala amesema polisi wamepiga picha nyumbani kwa Askofu wa Kanisa la Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima.

Kibatala ambaye ni wakili wa Askofu Gwajima amesema jana kuwa mbali na kupekuwa na kupiga picha kila kona walikwenda katika kanisa lake lililopo Ubungo.

“Waache wafanye yao na sisi tutafanya yetu kisheria. Kwani hatuwezi kuwazuia Polisi kufanya shughuli yao na baada ya kumaliza na sisi tutajua nini cha kufanya,” amesema Kibatala.

Msemaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, David Mngongolwa amesema Gwajima alikwenda jana kuripoti kama alivyoamriwa kufanya hivyo.

Mngongolwa amesema baada ya kuripoti askari walimchukua na kwenda naye nyumbani kwake wakakaa kwa dakika zisizozidi sita na kuondoka naye.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda amesema hana taarifa za kukamatwa kwa Gwajima kwa maelezo kuwa alikuwa katika kikao.

“Naomba uumtafute Sirro (Simoni-Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Gwajima awali alishikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam hivyo ni vema ukamtafuta kamishna,” amesema Kamanda Kaganda.

Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364