-->

Rose Ndauka Asema Aliumia Kuachana na Mpenzi Wake ‘Malick’ Siku Chache Kabla ya Ndoa Yao

Msanii wa filamu Rose Ndauka amesema hakuna kitu kilimuumiza katika maisha yake kama kuachana na mpenzi wake Malick Bandawe aka Chiwaman, siku chache kabla ya ndoa yao kufanyika.

Rose Ndauka Akiwa na Malik Mzazi Mwezie

Rose Ndauka Akiwa na Malick Mzazi Mwezie

Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Rose Ndauka amesema aliumia kwa sababu alishatangaza kwa watu, kwamba anatarajia kufunga ndoa.

“Kiukweli iliniumiza sana, kwa sababu mpaka tumefikia hatua tufunge ndoa, na nilikuwa naamini kuwa siku chache zijazo Rose sio Rose tena bali ni Mrs fulani,” alisema Rose. Lakini mimi naamini ndoa inapangwa na Mungu, ilipofika mwenyezi Mungu hakuhitaji kile kitu kifanyike, basi nikamshukuru Mungu,”

Rose alisema kwa sasa yupo kwenye mahusiano na mtu mwingine huku akidai kuwa hawezi kupata mtoto mwingine nje ya ndoa.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364