-->

Shilole Acha Figisu – Nuh Mziwanda

Baada ya video mpya ya Nuh Mziwanda ‘Jike Shupa’ kuachiwa na kuzua gumzo mitandaoni kutokana na namna msanii huyo alivyoweza kuelezea kisa na matukio yaliyokuwa yakimkuta alipokuwa akitoka kimapenzi na Shilole.

Mziwanda Akiwa na video queen wa kwenye video ya jike shupa

Mziwanda Akiwa na video queen wa kwenye video ya jike shupa

Nuh Mziwanda amedai toka kutoka kwa video hiyo mpenzi wake huyo wa zamani amekuwa akimpiga vita na kuwakataza baadhi ya wasanii wasimpe support msanii huyo kwa madai kuwa video yake hiyo imemdhalilisha, Nuh Mziwanda amemtaka msanii huyo kuacha roho mbaya na kumtaka afanye kazi aachane na mambo ya kiki kwani mashabiki wanataka kazi na si kiki anazotafuta yeye.

“Haya sasa habari zote nimepata unahangaika kuishusha ‘Jike shupa’ huwezi maana tunaishi chini ya Mungu na huwezi zuia nguvu ya mashabiki wangu ambao wapo tayari kwa chochote kwa ajili ya muziki wangu. Nahisi ulidhani nikitoka huko sitaendelea kimuziki dada naamini ndani ya kipaji changu. Na kingine nakushauri fanya kazi acha skendo hazina mpango kwani mashabiki siku hizi wanataka muziki mzuri maana stejini hauwezi imba skendo.” alisema Nuh Mziwanda

“Mama kua na roho ya kibinadam utafanikiwa acha roho mbaya na chuki.Mimi na deal na Mungu wangu na mashabiki wangu na naamini ndani ya kipaji changu na usipaniki sana huu mwanzo tu bado Ngoma nyingi kali zinakuja. Usipandikeze chuki kwa watu nakuomba”alisisitiza Nuh Mziwanda

 

 

NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

KAMA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364