-->

Wastara Afungukia Kuvunjika kwa Ndoa Yake na Mbunge Sadifa, Adai Kumempa Amani

Msanii wa filamu Wastara Juma amefunguka na kuzungumzia kuvunjika kwa ndoa yake na Mbunge wa Donge kupitia CCM Sadifa Khamis Juma ambayo imeduku kwa kakribani miezi 3.

WASTARA899

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Wastara amesema mahusiano ya mapenzi ni kama mtu anavyoishi na rafiki yake, mkizinguana maachana.

“Binafsi kwa sababu ni muda mchache naumia kuwakarahisha mashabiki wangu kwa sababu hawamchukulii Wastara katika stori hizo au katika muonekano huo,” alisema Wastara. Lakini kwa upande wangu naona ni bora zaidi nilivyotoka mapema kwa sababu pengine ingeniathiri nikashindwa kufanya kazi zangu na kulea wanangu,”

Wastara alisema hawezi kuzungumzia chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yake kwa kuwa yale ni maisha yake ya ndani.

Pia Wastara amesema bado umri wake unamruhusu kuingia tena kwenye mahusiano, ukifika wakati amempata mtu sahihi ataolewa tena.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364