-->

Wezi wa Filamu Kufungwa Jela Miaka Mitatu Faini Milioni 5

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) itaendelea na msako mkali kwa wafanyabiashara wote wanauza kazi za filamu na muziki bila kubandika stempu halali za kodi, ili kulinda kazi hizo kwa ajili ya kuwanufaisha wasanii pia kuhakikisha serikali inapata kodi kutoka na kazi za wasanii.

Bwana Kayombo akionyesha mfano wa bidhaa ya Filamu kwa wanahabari hawapo pichani.

Bwana Kayombo akionyesha mfano wa bidhaa ya Filamu kwa wanahabari hawapo pichani.

Msako endelevu utahusisha kukamata bidhaa zote ambazo hazina stempu za kodi na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika,kwa mujuibu wa sheria ya ushuru wa bidhaa kanuni za ushuru wa stempu kwenye Filamu na muziki 2012, watakaobainika watatozwa FAINI SIYOPUNGUA SHILINGI MILIONI TANO AU KIFUNGO KISICHOPUNGUA MIAKA MITATU JELA.

Msako huu unaendelea katika maduka yote kukagua bidhaa zote za filamu na muziki zilizotengenezwa kwa ajili ya biashara zibandikwe stempu za Kodi.

TRA inawatahadharisha wananchi wote kuwa makini wakati wa kunua bidhaa hizo wanunue bidhaa zilizobandikwa Stempu za ushuru wa kodi tu, kinyume cha hapo watoe taarifa katika ofisi yoyote ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pale mfanyabiashara anauza bidhaa ya filamu bila kubandika Stempu ya kodi.

Kazi zote ziwe za nje au hapa ndani zinatakiwa kubandikwa stempu za kodi, kuna rangi mbalimbali zinazobandikwa katika bidhaa, Stempu ya rangi ya kijani inabadnikwa katika filamu kutoka nje ya nchi.

Rangi ya Zambarau ni kwa ajili ya filamu zinazotengenezwa ndani ya Nchi na rangi ya Blue ni kwa ajili ya muziki kutoka nje huku rangi Pinki ni kwa muziki uliotengenezwa ndani.

Aidha katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo amewashauri wasanii na wadau wote wasiuze Haki zao za filamu kwani kwa kufanya hivyo hawatafaidika na jasho la kazi zao, waangalie njia nzuri ya kulinda kazi zao.

“Tunatoa wito kwa wasambazaji na wauzaji wa kazi za filamu na muziki ambazo hazina Stempu halali za kodi kuacha mara moja na kufuata utaratibu wa kupata Stempu hizo katika ofisi za TRA ili wawe na uhalali wa kuuza bidhaa hizo,”anasema Richard Kayombo.

FC

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364