Artists News in Tanzania

Donald Trump Ashinda Uchaguzi wa Rais Marekani

Donald Trump amemshinda Hillary Clinton katika matokeo ya uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.

trump34

Donald Trump

Bi Clinton amempigia simu Bw Trump kumpongeza kwa ushindi wake.

Bw Trump alikuwa ameshinda majimbo mengi muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda.

Alikuwa ameshinda Ohio, Florida, na North Carolina, ingawa Bi Clinton alishinda Virginia.

Kwa sasa Trump ana kura 265 za wajumbe na Clinton 218 kwa mujibu wa makadirio ya ABC News. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe.

Lakini mgombea wa Republican Bw Trump ameshinda majimbo mengi ya kusini mwa Marekani naye Bi Clinton akashinda majimbo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa makadirio ya shirika la utangazaji la ABC News.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, amemuandikia ujumbe wa kumpongeza Rais mpya wa Marekani Donald Trump baada ya kushinda na kuwa rais mpya wa nchi hiyo.

 

Comments

comments

Exit mobile version