Artists News in Tanzania

Picha: Uchaguzi wa Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania

1.Mgeni rasmi wa Shughuli hiyo,Waziri wa Habari,Utamadunina Wasanii,Nape Nnauye (katikati) akizungumza jambo katika hafala hiyo. Mgeni rasmi wa Shughuli hiyo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Mh. Nape Nnauye (katikati) akizungumza jambo wakati wa zoezi hilo. Mpinzani wa Mwakifwamba, Issa Hamis Kipemba (mbele) akizungumza jambo kabla ya uchaguzi kuanza. Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania aliyekuwa akimaliza mda wake, Simon Mwakifwamba (kulia) na Makamu wake, Deosonga Njelekela wakiwa mbela kujinadi kuomba kura kwa wapiga kura wao. Baadhi ya wajumbe kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wakifuatilia kwa makini taratibu zilizokuwa zikitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi. Wasanii wa vichekesho hapa, Mkwere (wakwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Chama Cha Komedi nchini Sumaku wakifuatilia uchaguzi uliokuwa ukiendelea. Muigizaji Mkongwe wa Filamu, Mzee Chilo (kulia) akifuatilia kwa makini uchaguzi uliokuwa ukiendelea. Wagombea wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Nape, kabla ya uchaguzi kufanyika. Wajumbe wakipiga kura kuwachagua viongozi wao. Wajumbe wakiweka karatasi za kura katika masanduku maalum yaliyokuwa yameandaliwa. William Mtitu akiweka karatasi yake kwenye sanduka maalum baada ya kupiga kura. Single Mtambalike akiweka kura yake ndani ya sanduku la kura.Waliopo mbele ni baadhi ya viongozi walichaguliwa wakiwa katika picha.

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba jana alishinda tena kiti hicho kwa kupata kura 47 za ndiyo kati ya 50 zilizopigwa kwenye uchaguzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa Urafiki uliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kura tatu za hapana zimepatikana huku mpinzani wake akijitoa kwa madai kuwa hakukuwa na maandalizi mazuri ya uchaguzi huo.

PICHA NA DENIS MTIMA/GPL

Comments

comments

Exit mobile version