Artists News in Tanzania

Picha: Wasanii na Viongozi wa WCB Wakiwa Nyumbani kwa Rais Mtaafu Jakaya Kikwete

Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete Jumatano hii aliwaalika wasanii wa label ya WCB pamoja na viongozi nyumbani kwake na kula nao chakula cha mchana.


Diamond na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete

JK ambaye ni mmoja kati ya marais ambaye amesupport sana wasanii wa muziki nchini, aliwaalika wasanii hao nyumbani kwake na kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu muziki wao.

Mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Sallam alimshukuru rais huyo kwa kuwaalika nyumbani kwake na kuzungumza nao mawili matatu kuhusu muziki.

“Former President JM Kikwete and Former First Lady Mama Salma Kikwete. Asanteni kwa mwaliko wenu!! Allah awape afya njema,” Sallam aliandika instagram.

Wasanii wa WCB pamoja na JK


Mavoko akimkabidhi JK CD ya wimbo wake

Bongo5

Comments

comments

Exit mobile version