Artists News in Tanzania

Video Mpya ya Diamond Kuzinduliwa Leo

VIDEO mpya ya msanii wa kizazi kipya nchini, Nassib Abdul, ‘Diamond Platnum’, ‘Make me Sing’, inatarajiwa kuzinduliwa leo itakapochezwa kwa mara ya kwanza katika  televisheni ya MTV Base.

Diamond, anayetarajiwa kwenda nchini Marekani kufanya kazi na mtayarishaji wa muziki, Swizz Beat pamoja na kupiga picha za video yake aliyomshirikisha Neyo, katika video hiyo amemshirikisha mkali kutoka Afrika Kusini, A.K.A.

Hivi juzi kati kupitia ukurasa wake mtandaoni, Diamond aliandika;

FRICA!!!! i know you been waiting for this…and it’s ready for You!… TANZANIA + SOUTH AFRICA = HIT?… this Friday! #12022016
( kwanza kabisa ningependa kumshkuru Mwenyez Mungu kwa kuweza katusaidia kufanikisha ndoto zetu za Bongo falvour kuweza kuingia na kupata nafasi nzuri West africa… kama nilivyoahidi na kuzungumza mwanzo kuwa mwaka huu Moja ya Mission zangu ni kuhakikisha pia Muziki wetu unapata nafasi nzuri South Africa na America… tafadhali usiache kunisupport ili kwa pamoja tuufikishe mziki wetu Kileleni…) #MakeMeSing @akaworldwide X @DiamondPlatnumz Drops on Friday!

Comments

comments

Exit mobile version