Artists News in Tanzania

Waziri Amtaka Gardner Aombe Radhi Kwa Kumdhalilisha Lady Jaydee

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla, amemtaka mtangazaji wa Clouds FM, Gardner G Habash kumuomba radhi aliyekuwa mke wake, Lady Jaydee kwa ‘kile alichokiita’ kama udhalilishaji kwake na kwa wanawake wote.

Wikiendi iliyoisha imesambaa video mtandaoni ikimuonesha mtangazaji huyo akiongea kwenye tamasha alilokuwa mshereheshaji: My name is Captain Gardner G Habash all the way from Clouds FM, Jahazi hatari sana. Na sina neno na yule mtoto wa kike. Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi.”

Video hiyo imesababisha hasira kubwa kwa mashabiki wa Jaydee na watu wengi kwa ujumla.

Bongo5

Comments

comments

Exit mobile version