Afande Sele: Bongo Fleva Imefuata ya Bongo Movie
Rapper mkongwe kwenye bongo Fleva, Afande sele, amesema muziki wa bongo fleva sasa hivi unapoteza dira na kufuata nyayo za bongo movie, za kutumia kiki kutangaza kazi.
Akiongea kweye Planet Bongo ya East Africa Radio, Afande Sele amesema masuala ya kiki yalikuwa ni kawaida kwa wasanii wa filamu za bongo, lakini sasa hivi wasanii wa bongo fleva pia wanafuata nyayo hizo.
“Kwenye bongo movie miaka yote imekuwa iko hivyo kwa sababu hakuna mtu aliyefanya kazi nzuri kwenye bongo movie, hakuna mtu wa bongo movie amabye unaweza kusema huyu tunamjua kwa ajili ya kazi zake bora, isipokuwa tunamjua kwa sababu ana kashfa fulani kwenye magazeti, ana skendo fulani, kwa hiyo na bongo fleva nao wanaingia kwenye kundi hilo la kkibongo movie”, alisema Afande Sele.
Afande Sele ambaye pia alijaribu kutupia karata yake kwenye siasa, amesema pia wasanii wa bongo fleva sasa hivi wanashindwa kutumia kazi zao kujitangaza, na hatimaye kuangukia huko kwenye kiki.
eatv.tv