-->

Alikiba Ampagawisha Waziri Nape Nnauye

Msanii Alikiba ambaye leo ameachia remix ya wimbo wake wa ‘Aje’ ameonesha kumkosha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kiasi cha Waziri huyo kusema kuwa Alikiba ni kati ya wasanii wanaofanya ajisikie fahari kuwa Waziri

Mh. Nape Nnauye

Mhe. Nape Nnauye amesema hayo leo baada ya msanii huyo kukabidhiwa tuzo yake katika kituo kimoja cha Television nchini Afrika Kusini na kuachia kazi yake mpya ambayo imeonesha kuwakosha watu wengi.

“Kiba! Big Up! Am so proud of you! we ni mmoja wa wasanii wanaonifanya nijisikie fahari kuwa Waziri wa Sanaa Tanzania! May allah bless you!” aliandika Nape Nnauye 

Msanii Alikiba ni kati ya wasanii wachache kutoka Tanzania ambao wanaiwakilisha vyema nchi kupitia muziki wao.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364