-->

Alikiba Amzungumzia Chid Benz na Sakata la Dawa za Kulevya

Msanii Alikiba amejitosa kwenye suala la dawa za kulevya kwa kumtetea aliyekuwa swahiba wake Chid Benz kwa kusema anapofungwa mtumiaji wa dawa za kulevya ni kumtesa bali anapaswa kupelekwa katika vituo vya afya ili aweze kupatiwa tiba mbadala.

Alikiba ameeleza hayo baada ya Chid Benz kukamatwa na dawa za kulevya hivi karibuni na Jeshi la Polisi na kuweka chini ya uangalizi mkali wa Mahakama jambo ambalo watu wengi walishtushwa na taarifa hizo kwa kuwa walitegemea pengine atabadilika tabia hiyo alivyotoka ‘Rehab’.

“Unapomfunga mtu ambaye ni mtumiaji wa dawa za kulevya ni mateso makubwa kwa kuwa mtu huyo anapaswa apelekwe kitengo maalum ili apatiwe dawa za kuzuia kutamani vitu vya aina hivyo, pia yeye mwenyewe tunapaswa tumshauri ili aweze kushinda nafsi yake. Ujue vitu kama hivyo ni kuishinda tu nafsi katika kuamua na akae navyo mbali.
Pamoja na hayo, Alikiba aliendelea kwa kusema “kama ametoka ‘Rehab’ hivi karibuni halafu inasemekana amejihusisha tena na hivyo vitu ni makosa makubwa kwa sababu tayari umetoka katika kupata tiba halafu unayakaribia tena hiyo haifai kabisa”, alisema Alikiba.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364