Alikiba apewa jina jipya Uingereza
Mtandao mkubwa wa kuuza muziki wa TIDAL ambao upo chini ya rapa Jay Z umempa jina jipya msanii kutoka Bongo Alikiba na kumtambua kwa jina la ‘The unstoppable’ yaani mtu asiezuilika kwa kitu akifanyacho.
“The unstoppable AliKiba is live right now in London” mtandao wa TIDAL uliandika wakati Alikiba akifanya yake kwa steji usiku huo.
Alikiba alipewa jina hilo wakati akishiriki katika moja ya tamasha la muziki ambalo lilifanyika mwisho wa wiki nchini Uingereza ambalo lilikusanya mastaa kibao akiwepo Cassper Nyovest, P Square, Davido, Awilo Logomba, Sarkodie, Tekno , MI na wasanii wengine wengi huku bongo ikiwakilishwa na ‘King’ Alikiba ambaye alipata nafasi ya kufanya ‘performance’ ya ngoma zake kama Mwana, Unconditionally Bae na Aje.
Mashabiki wengi wameonyesha kufurahishwa na hatua hiyo ya Alikiba kushiriki katika tamasha hilo kubwa huku akiwa na wasanii wakubwa kibao, kwani wanaamini jambo hilo linazidi kumjenga na kufungua njia zaidi katika kazi yake hiyo ya muziki.
EATV.TV